Habari na picha na Rajabu Mwenda

Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Mheshimiwa Dr Seif S. Rashid alisema juzi siku ya jumamosi 02/02/2014 katika msikiti wa kichangani magomeni Dar-es-salaam ambako alikuwa mgeni rasmi katika zoezi la kuchangia damu ambalo liliratibiwa na Mpango wa Taifa wa damu salama kanda ya mashariki kwa kushirikiana na Jumuiya ya akhlaaqul Islaam (JAI) 

Akisoma hotuba kwa niaba ya waziri wa afya kaimu mkurugenzi wa tiba wizara ya afya Dr Hadiel senkoro alisema, viongozi wa dini, tasisi za serikali, mashule na vyuo waige mfano mzuri wa Jumuiya ya akhlaaqul islaam wa kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya mama na motto. 

Waziri alieleza unapotoa damu, unachangia kuokoa maisha ya Watanzania wengine na hata ya ndugu yako wa karibu. watumiaji wakubwa wa damu ni watoto chini ya miaka mitano hasa wenye upungufu wa damu (50%), akinamama wenye matatizo wakati wa ujauzito(30%) na wahanga wa ajali(15%). 

Baadhi ya vifo vinaweza kuepukika kama hospitali zetu zitakuwa na damu salama ya kutosha.Takwimu zinaonyesha kuwa uvujaji wa damu wakati wa uzazi unachangia asilimia 44% ya vifo vya kina mama katika nchi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara. 

Ni dhahiri kuwa damu salama ikiwepo wakati wote inapohitajika itapunguza kwa kiasi kikubwa vifo hivi. Waziri aliwatoa shaka watu wanaoogopa kuchangia damu hakuna madhara yoyote yanayotokana na kuchangia damu. 

Binadamu ana ujazo wa damu wastani wa lita 5. Kiasi kinachochukuliwa wakati wa kutoa damu ni kidogo sana hata nusu lita haifiki (450 ml). Ujazo wa damu katika mwili hurudia hali ya kawaida ndani ya masaa 36. 
Katika zoezi hilo ambalo lilifanyika kwa siku mbili jumla ya chupa za damu 288 zilikusanywa ambazo zitapimwa na kusambazwa katika hospitali mbalimbali mkoa wa Dar-es-salaam
Meneja wa mpango wa Taifa wa damu salama Dr Efesper Nkya akitoa neno la shukrani. Kulia kwake ni mkurugenzi wa tiba wizara ya afya Dr Hadiel senkoro ambaye alimwakilisha Waziri wa Afya wakati wa zoezi la kuchangia damu katika msikiti wa kichangani magomeni Dar-es-salaam
Mmoja wa wachangiaji damu
Kinamama nao walikuwa mstari wa mbele kuchangia damu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Muumba awalipe, damu ni muhimu sana. GREAT CREATIVITY MASHAALLAH

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...