Raia wa Ugiriki, Alexamdrios Atanasios, amekamatwa maafisa wa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumapili usiku Februari 24, 2014, akiwa na kilo tano za madawa ya kulevya.
Habari zinasema mzungu huyo alikamatwa wakati wa upekuzi, akijiandaa kupanda ndege ya Swiss air kueleke jijini Zurich, Uswisi.
Madawa hayo yalikutwa yakiwa yamefichwa kwenye “sakafu” ya begi lake baada ya mitambo ya kisasasa yaupekuzi, kugundua kuwa kulikuwa na ‘mzigo’.
Habari zinasema, kwa sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha uwanjani hapo akisubiri taratibu za kisheria ili afungukliwe mashtaka.
Kautoa wapi? Again hatuwezi kuua mmbuyu kwa kukata matawi.lazima kuongoa mizizi.Hawa punda wanaoshikwa kwenye Airports kunawanao wamiliki.
ReplyDeleteHiyo Henellic ni nchi gani wajameni?
ReplyDeleteGood work to the airport personnel in finding the 'unga wa kulevya'. You deserve a bonus. Hili lijamaa must have thought that atapita tu maana wafanyakazi wa airport wapo wapo tu. But he was not so lucky THIS time eh!!
ReplyDeletehiyo nchi ndio kwanza naisikia
ReplyDeleteKwanini mmetoa picha yake hadharani?Si mtaaribu upelelezi wenu au?(Utani.....)?.Kama alivyosema mwana blog ya jamii hapo juu,aliutoa/nunua soko gani?
ReplyDeleteDavid V
Jamani tumechoka kuonyeshwa wanaokamatwa kisha hatusikii mwisho wa hiyo taarifa, yule mke wa kigogo aliekamatwa na kete kaziweka kichani kaishia wapi na wengine wengi. Mdau wa hii blog hebu fanya uchunguzi utuhabarishe kinachoendlea katika hizi kesi za madawa ili hata hawa wanaotaka kuendeleza waogope kwa kigezo cha hao walio kamatwa
ReplyDeleteKule Oman yule Zahoro matelephone kesi yake ilikwenda siku 5 tu , hapa kwetu kesi za unga zinachukuwa miaka na miaka tokea mtoto amezaliwa mpaka anaanza shule ya msigi kesi hazijahukumiwa lengo lake hasa silijui ni Hongo au nini? nchi imeoza kweli hii
ReplyDeleteisije kuwa ulikuwa wa matumizi yake binafsi
ReplyDeleteAfadhali ulikuwa unatoka kwenda nje ya nchi kuliko kuingia nchini! lol
ReplyDeletetusubiri tuone hii issue itaishia wapi
ReplyDeleteJamani isije kuwa kabeba kwa matumizi yake binafsi
ReplyDeleteHaya mambo ya unga yamezidi kabisa. Ukiangalia athari zake zinatisha.
ReplyDeletehukumu ya sembe kiasi hicho huko kwao ugiriki ni kifungo cha maisha nayeye apewe hocho hicho hapo
ReplyDelete