Bondia wa ngumi za kulipwa Fadhili awadh amefariki dunia katika hospital ya Mwananyamala jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa siku kadhaa. 
Marehemu Fadhili Awadh alikuwa ni miongoni mwa mabondia waliochaguliwa kucheza  mpambano wa ubingwa tarehe 29 mwezi huu wa tatu dhidi ya mpinzani wake toka Tanga Alan Kamote, na  alikuwa katika maandalizi ya mpambano huo. 
Sababu ya kifo chake kwa ripoti ya daktari wa Mwananyamala kwa kiongozi wa ngumi Ibrahim Kamwe ni kuwa fadhili alikuwa na malaria na alitumia dozi ya metakelfin, na hali ilibadirika pale alipojaribu kufanya  mazoezi na kujisikia vibaya na kuwahishwa katika hospitali hiyo ambayo alikaa kwa siku mbili akiendelea na matibabu na hatimae umauti ulipomkuta. 
Fadhili awadh mwenye umri wa maika 32 alikuwa anaendelea vizuri katika mchezo huo kiasi cha kufikia kucheza pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA sabsaba, akiwasindikiza mabondia Japhet Kaseba na Thomas Mashali. 
Shughuli za maazishi zinafanyika nyumbani kwao maeneo ya manzese.
Sisi tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi,
Ailaze roho ya marehemu Fadhili awadh “Tiger” peponi 
 AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pigo kwa familiya na Taifa kwa ujumla.
    Mungu amlaze mahala pema.

    ReplyDelete
  2. Hizi dawa za Metakelfin mbona zina matatizo sana? kwanini Serikali isizipige marufuku? Kuna jamaa mwinginea amegeuka kuwa mlemavu wa ngozi baada ya kunya hizi metakelfin.
    Mungu amlaze mahala pema peponi marehemu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...