
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewafukuza kazi askari wake wanne waliodhibitika kujihusisha na matukio ya uhalifu, kwa mujibu wa Kamanda wa kanda hiyo Kamishna Suleiman Kova (pichani).
Kamanda Kova amesema leo jijini kuwa hatua hiyo imekuja baada ya uchunguzi wa awali kubaini kuwa askari hao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uhalifu.
Ameseme vitendo hivyo ni pamoja na tukio la Machi 9, 2014 ambalo lilitokea eneo la Mbezi beachi A jijini Dar es salaam ambapo majambazi wapato 15 walifika katika ofisi za kampuni ya Kichina ijulikanayo kwa jina la Hongyang na kupora vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha taslimu na simu na kisha kutoweka.
Kamishina Kova amesema kuwa askari hao wanaotoka katika vikosi mbalimbali ni pamoja na aliyekuwa koplo Rajabu Mkwenda mwenye namba E6396 aliyekuwa askari wa makao makuu Polisi, F9412 PC Saimon wa kituo cha polisi kati, F9414 PC Albanus Poosa wa kikosi cha bendi ya polisi Dar es salaam, na F9512 PC Selemani wa kituo cha polisi kigamboni.
Aliseme watu hwao wanastahili adhabu hiyo na hatua zingine zinazofuata kutokana na vitendo hivyo, na kwamba wao kwa sasa sio polisi tena na wanakosa haki zao zote.
Kamanda Kova aliongeza kuwa katika kuhakikisha haki inatendeka katika suala hilo, watuhumiwa wote hao wametambuliwa na mashahidi na kwamba taratibu za kipelelezi zilidhibitisha kujihusisha kwao na majambazi ambao ni raia.
Kamishina Kova amesema jeshi hilo lipo katika hatua za kujisafisha ili lionekane ni jeshi bora na zuri mbele ya wananchi.
Wafukuzwa bila ya kuwafungulia manshtaka? Raha unavamia pahala ukikamatwa unafukuzwa Kazi tu.
ReplyDelete