Baada ya kutokea vurugugu zilizosababishwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum kupelekea Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Warioba  (pichani juu, akiongozwa kutoka Bungeni baada ya zoezi la kuwasilisha rasimu ya katiba kuahirishwa) kutokuwasilisha rasimu ya pili ya Katiba kwa wajumbe hao, Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta aliitisha kikao cha maridhiano na baadhi ya wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali yaliyopo katika Bunge hilo ili kupata muafaka wa hoja zilizokuwa zimejitokeza.
Baada ya kikao hicho kilichodumu kwa takribani masaa manne na kumalizika saa nne za usiku, Mhe. Samuel Sitta amewaeleza waandishi wa Habari matokeo ya kikao hicho, ambapo wajumbe wa kamati hiyo wameafikiana yafuatayo:

  1. Kikao cha Bunge Maalum kitaendelea kesho tarehe 18 Machi, 2014 Saa tatu asubuhi kwa kuanza na shughuli za kuapisha baadhi ya wajumbe ambao hawakuapa awali kwa muda wa dakika 30
  2. Kuhusu muda wa kuwasilisha Rasimu ya Katiba, Wajumbe wameafikiana Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Warioba kuwasilisha Rasimu ya pili ya Katiba kwa wajumbe hao kwa muda wa saa nne badala ya saa mbili alizokuwa ametengewa awali, ambapo uwasilishwaji wa rasimu huo utaanza rasmi saa tatu na nusu asubuhi baada ya shughuli ya viapo kumalizika.
  3. Saa kumi kamili jioni kutakuwa na semina ya kanuni itakayofanyika katika Ukumbi wa Bunge ambapo Mwenyekiti wa iliyokuwa kamati ya kanuni Mhe. Prof. Costa Mahalu na wenzeke watawawezesha wajumbe kupitia vifungu vya kanuni hizo za Bunge Maalum, ambapo semina hiyo itaendelea hadi jumatano tarehe 19 machi, 2014
  4. Siku ya Alhamisi tarehe 20 Machi, kutakuwa na semina itakayoendeshwa na maafisa wawili kutoka kenya ambao watatoa uzoefu wao katika maeneo haya.
  5. Aidha wajumbe wamekubaliana Mhe. Rais kulihutubia Bunge siku ya Ijumaa jioni kama ilivyokuwa imepangwa awali, ambapo asubuhi kutatanguliwa na shughuli za Mwenyekiti wa Bunge Maalumu kuunda kamati 14 za Bunge Maalum.
 News alert hii imeletwa na 
Owen Mwandumbya Kutoka Sekretariet ya Bunge Maalum
Kwa picha zaidi baada ya hapo BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Michuzi, mbona unaleta habari zisizo na viwango?

    Maana picha uliyotundika inaonekana watumishi wa Bunge Maalum wenye sare ni kama vile wanataka kumkokota nje Mheshimiwa Jaji Warioba!

    Je hali hii ktk picha ilitokana na nini mpaka pichani inaonekana kama watu wanataka kukokotwa nje ya Bunge hili Maalum la Katiba.

    Michuzi, fanya juu chini utuhabarishe maana wengine hatuna TV au tupo ktk diaspora na Globu ya Jamii ni zaidi ya BBC, CNN, AlJazeera, RussiaTV(RT).

    Mdau
    Dozi Kila Siku ya Globu Ya Jamii

    ReplyDelete
  2. Heri mie sijasema!

    ReplyDelete
  3. Najua wanataka kuvuta muda ili posho iongezeke. Ningekuwa na uwezo ningewatimua wote, sijui nani kawaleta hapo?

    ReplyDelete
  4. BUNGE SIO BAA WALA KLABU YA USIKU:

    BUNGE HASA LA KATIBA SIO KAMA MASKANI, KWA PUSHA WA BANGE AMA BANDA LA GONGO AU KIJIWENI:

    WAONGOZA BUNGE KAMA MHE. WARIOBA NA MHE. SITTA SIO MAUZA GONGO AMA MAPUSHA WA BANGE:

    BUNGE NI KAMA MSIKITI AMA KANISA KWA KUWA LINA KANUNI ZAKE NA TARATIBU ZAKE:

    Kwa nini pasiwepo na PINGU NA SELO BUNGENI?

    Ahhhh ninafikia kuichukia Siasa kwa mambomya kijinga kama waliyoonyesha Wawakilishi wetu waliteuliwa kwa heshima kubwa na Mhe.Raisi Kikwete.

    Hamuoni ya kuwa huo uwakilishi ni heshima kubwa sana kupewa?

    Wangapi wenye sifa na heshima zao hawakupata nafasi hiyo?

    Au mlitaka Raisi Kikwete awapime afya ya akili kabla ya kuwateua?

    Inawezekana wengi wenu ni Mitambo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...