Kufuatia mpango kabambe wa kuelimisha jamii dhidi ya makosa mtandao tayari kumekua na video za katuni, Mchezo wa komputa “Computer gane”, majarida ya katuni pamoja na machapisho mengine yote yakiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya jinsi ya kujilinda dhidi ya makosa mtandao kuanzia ngazi ya mtu binafsi hadi kufikia ngazi ya kitaifa.
Picha: Mfano wa Vijarida vinavyo toa elimu dhidi ya usalama mtandao.
Aidha, Bwana. Yusuph Kileo ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuangalia kwa karibu namna itakavyo unganisha nguvu kuhakiki jamii ya watanzania inatambua kwa kina maswala ya husuyo uhalifu mtandao pamoja ulinzi mtandao. Kileo aeleza ni vyema maswala yaha ya uhalifu mtandao yanayoshika kasi sana kwa sasa yanatazamwa kwa karibu ili kuhakiki jamii ya watanzania inabaki salama kimtandao.
Link: Mfano wa Video za Katuni zinazotoa elimu ya usalama mtandao.
Athari za makosa ya kimtandao ni kubwa sana endapo hatua za msingi za kudhibiti uhalifu mtandao hazitochukuliwa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi hadi taifa kwa ujumla. Mataifa makubwa tayari wamesha yaona haya na sasa kumekua na jitihada mbali mbali zenye malengo ya kukabiliana na uhalifu mtandao.

Kwa upande mwingine bwana Yusuph kileo ameasa vijana kuwa na juhudi ya kusomea maswala ya ulinzi mtandao kutokana na uhaba mkubwa ulioko wa wataalamu wa maswala ya ulinzi mtandao katika ngazi za dunia huku akitolea mfano mataifa makubwa kuanza kutengeneza majeshi mahususi yatakayokuwa yakikabiliana na vita mtandao “Cyber war”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...