Meneja wa Usafirishaji wa Kampuni ya Azam,Bw. Omari Said (kushoto) akipokea funguo za Fuso mpya kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Diamond Motors,Bw. Vikram Verma wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.anayeshuhudia Katikati ni Meneja Mkuu wa Diamond Motors,Bw. Martin Laurian.
Sehemu ya Fuso hizo.

Kampuni ya Bakhresa Group - maarufu kwa jina la Azam – ni kampuni ya kwanza ya wateja wa muda mrefu wa Diamond Motors (Hansa) kuthibitisha kuagiza Fuso mpya – ambayo sasa ni ya Kampuni ya Daimler.

Diamond Motors Limited, msambazaji pekee wa malori ya Fuso nchini na Kundi la Kampuni za Bakhresa wamedumisha uhusiano wa kibiashara wa muda mrefu na wenye faida kwa pande zote mbili kwa miongo miwili. Kampuni zote mbili zimejenga sifa imara kwa kusisitiza kwenye bidhaa zenye kiwango bora zaidi na huduma bora. Azam imekuwa bidhaa inayopendwa kwa matumizi ya nyumbani kwa miaka mingi na zinafahamika zaidi kwa ubora wa bidhaa zao.

 Fuso kama jina maarufu la lori limekuwa linafahamika sana kwa madereva na wamiliki wengi wa malori. Malori ya Mitsubishi Fuso ya kati na makubwa yanayomilikiwa na Daimler yametengenezwa kwa kuzingatia viwango sahihi zaidi.

Nchini Tanzania, sekta ya usafirishaji inatoa mchango mkubwa na muhimu hasa katika malengo ya Kilimo Kwanza kwa kuwa ardhi kubwa ya kilimo ipo pembezoni ambako kufikika kwake kunaweza kuwa changamoto kubwa kutokana na mtandao wa barabara usioendelezwa..

Kukabiliana na tatizo hili, Mr. Omar Said Athumani, meneja wa usafirishaji wa Azam amesisitiza umuhimu wa kuwa na mshirika anayefaa kutimiza mahitaji yao ya usafirishaji. “Bakhresa Food Ltd (BFPL) inasafirisha na kuuza Msumbiji, Malawi, Zambia, Uganda, Burundi na Tanzania kwa kutumia malori yake. Bidhaa zetu zote zipo kwenye kundi la bidhaa zinazoharibika haraka.

Mifumo yetu ya usambazaji inatakiwa iwafikie wauzaji wetu wa jumla na mlaji kwa wakati bila dosari. Bidhaa zinaharibika haraka zinazingatia muda na halijoto. Pamoja na kuunganisha michakato mingi kutoka sehemu nyingine katika Bakhresa Group, Bakhresa Food pia kushirikiana na wakulima wenyeji wa Tanzania kuzalisha matunda kwa matumizi kwenye kitengo utengenezaji wa juisi. Ni lazima matunda haya yafike kiwandani kwa wakati.

Baada ya hapo, bidhaa zitakazozalishwa ni lazima ziwafikie wauzaji wa rejareja kwa kutumia mifumo yao mikubwa ya usambazaji. Bakhresa Food inamiliki malori 200 kwa jumla, huku nyingi ya malori hayo zinatumika kwenye kitengo cha maji. Kwa hiyo unaweza kuelewa kiwango cha ufanisi na mategemeo yetu kwa malori ya Fuso.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...