Kampuni ya EMOC imetoa msaada Kwa watoto yatima katika kituo cha New Life Orphanage Home kilichopo kigogo ambacho ni makao makuu ya kituo cha watoto yatima. New Life Orphanage Home ni kituo ambacho kimejitolea kulea watoto yatima wasiojiweza tangu mwaka 1998.

New Life Orphanage Home kilianzishwa Magomeni mwaka 1998 Kwa lengo la kusaidia watoto yatima, na kilianza na watoto 18 tu. New Life Orphanage Home kimefanikiwa kufungua kituo kikubwa zaidi Kigogo iliopo wilaya ya Kinondoni na kuwa na idadi ya watoto 101 kuanzia watoto wachanga wa miezi hadi watoto wanapopata kazi.

“Kipindi hiki Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhudumia watoto wasiojiweza wakiwemo yatima ambao wazazi wao walifariki wengine kwa magonjwa. Kuna namba kubwa ya watoto yatima wasiojiweza na wengina kuwa mitaani bila msaada wowote.

Kuna vituo vichache sana ambavyo vilianzishwa na watu binafsi katika kusaidia watoto wasiojiweza. Kimoja wapo ni kituo cha New Life Orphanage Home ambacho kimejitolea kulea watoto kuanzia miezi mpaka wanapoolewa kwa wasichana na kupata kazi kwa wavulana.
Kutokana na matatizo yanayowakabili watoto yatima, Excel Management and Outsourcing (T) Limited imeamua kutoa msaada kwa watoto yatima katika kituo cha New Life Orphanage Home kila baada ya miezi mitatu. Kampuni ya EMOC imeona ichukue nafasi hii ndogo kutoa msaada kwa watoto yatima wa kituo cha New Life Orphanage Home kwa kila baada ya kipindi cha miezi mitatu ikianza leo hii tarehe 28.03.2014”.

  “Japo msaada sio mkubwa sana kukidhi mahitaji ya watoto yatima,bali itasaidia kidogo kufanya watoto wajisike wapo kama watoto wengine wenye wazazi, wanapendwa na watu wote wanaowazunguka na pia kupata haki zao za msingi za kulelewa kama watoto wengine kwa wazazi wao” Excel management and Outsourcing (T) Limited Ni Kampuni ambayo imejikita kutoa huduma East Africa Yote ikiwa na malengo ya kufungua matawi katika mikoa ya Arusha na Mwanza. Kwa hapa Dar es Salaam imetanua mabawa yake Kwa makapuni zaidi ya 50.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...