Mfanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Zabida Kibiki akimvisha shuka baada ya kumkabidhi msaada huo John Shitundu ambaye ni miongoni mwa wazee waliopo chini ya kituo chaTushikamane Pamoja Foundation wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa kituo hicho Rose Mwapachu.
 Meneja Mikataba wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Taddious Theodore akimkabidhi  msaada wa Shuka Julieth Mchanga  kwa niaba ya wazee wenzake 45,  wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walitembelea kituoni hapo kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam, vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia  chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  wakiwa katika picha ya pamoja na wazee wasiojiweza wa kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation ilichopo Yombo Kilakala wakati walipokwenda kuwapa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mashuka, blanketi,vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 2.5
 .Wafanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  wakiwa na mizigo mbalimbali ya vyakula wakati  walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika eneo la Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,  wanaolelewa na Kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchere na mafuta ya chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
Baadhi ya wazee wanaoishi na kutunzwa katika Kituo cha  Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,wakicheza pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  walipowatembelea wazee hao mahususi kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...