Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtwisha ndoo ya maji Bi. Amina Rajab, mkazi wa Wilayani Mpwapwa, baada ya kuzindua rasmi Kisima cha Bomba la maji, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi Kisima cha Bomba la maji sikiliza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. Kushoto kwa Makamu ni Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe,(kushoto) ni Mama Asha Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Maji wa Wilaya ya
Mpwapwa, Shadrack Matemba (wa pili kulia) wakati alipotembelea moja ya
chanzo cha maji wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji
zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19,
2014. Kulia kwa Makamu ni Mama Asha Bilal na Waziri wa Maji , Profesa
Jumanne Maghembe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wagogo wakati alipokuwa akiwasili katika sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.
Baadhi ya wananchi wa Wilayani Mpwapwa wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akiwahutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.Picha na OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...