Meneja uwanja wa ndege wa Songwe jijini Mbeya, Eng. Valentino Kadeha (Kulia) akitoa maelekezo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea Mradi huo. Kwa Mujibu wa Mhandisi Kadeha Uwanja huo umeshakamilika kwa aslimia 70 na utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria zaidi ya 300 kwa saa.
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr  Sankey (Wapili Kulia) akieleza changamoto zinazozikabili Hospitali hiyo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pia ilipotembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya. Aliyeambatana nae ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Humphrey Kiwelu (Kulia).
 Kiongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye nguo nyeusi) akionja maji kutoka moja ya njia za kusambazia maji ya Mradi wa Maji wa Iwalanje. Kukamilika kwa Mradi huo kumetoa suluhisho la adha ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa Kijiji cha Iwalanje na Taasisi mbalimbali za Serikali zinazohudumiwa na Mradi huo.
Ukaguzi wa Hospitali.. Kwa kutambua umuhimu wa afya kwa maendeleo ya nchi, Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pia ilitembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya. Timu hiyo ilishuhudia maendeleo ya ujenzi wa jengo la Kitengo cha Dharura (linaloonekana nyuma). Kwa  habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mipango ya maendeleo ni mizuri, ila itekelezwe ili wananchi wafaidike.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...