Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali katika Bunge la Pamoja la Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) na Jumuiya ya Ulaya leo jijini Strasbourg Ufaransa. 

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) akipitia hotuba yake kabla ya kuhutubia Bunge la Pamoja la Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) na Jumuiya ya Ulaya leo Strasbourg Ufaransa.  Mhe. Mchemba anaongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho na ameitaka Jumuiya ya Ulaya kuacha kushinikiza nchi za ACP kuweka sahihi Mikataba ya Ubia wa Biashara ambayo haina tija kwa nchi za ACP. Kulia ni Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala na kushoto ni Bi. Raymold Dominic Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya ACP anayesimamia masuala ya siasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tafadhali,kama kuna video,tungependa kuangalia na kusikiliza tujue tulivyowakilishwa.

    ReplyDelete
  2. tuwekee video tuone ili watu wasiwe na maswali ya kizushi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...