Ndege ya Malaysia iliyotoweka Mkuu wa jeshi la anga la Malaysia, amekanusha madai kuwa ndege ya Malaysia iliyotoweka, ilionekana mara ya mwisho Magharibi ya rasi ya nchi hiyo, eneo ambalo ni mbali zaidi na njia iliyostahili kupita.


Generali Rodzali Daud, amesema kuwa hawawezi kupuuza uwezekano huo, lakini amesema madai kuwa mawasiliano ya ndege hiyo yalinaswa na mtambo wa radar katika eneo hilo sio kweli.

Amesema mawasiliano ya mwisho ya ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing yalinaswa katika rasi iliyoko kati ya Malaysia na Vietnam.

Ndege na meli kadhaa zimekuwa zikitafuta mabaki ya ndege hiyo katika eneo la bahari ya Malaysia, lakini hazijafanikiwa kupata mabaki ya ndege hiyo.

Ndege ya Malaysia iliyotoweka kabla ya
kutoweka siku ya Jumamosi.
Msako unaendelea Jeshi la Malaysia limesema kuwa, mtambo wake wa radar unaashiria ndege hiyo iliyotoweka, ilielekea eneo la Magharibi, mbali na njia iliyostahili kupita kabla ya kutoweka. Ndege hiyo MH370 ilitoweka siku ya Jumamosi, baada ya kupaa ikiwa na abiria mia mbili na thelathini tisa.

Juhudi za kimataifa za kutafuta ndege hiyo zimepanuliwa na kuimarishwa. Awali ilibainika kuwa watu wawili waliokuwa wakisafiri kwa kutumia paspoti zilizoibiwa walikuwa raia wa Iran ambao hawana uhusiano na kundi lolote la Kigaidi.
Ndege ya Malaysia iliyotoweka kabla ya kutoweka siku ya Jumamosi.

Chanzo BBC Swahili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AINA YA NDEGE NI BOING 777 NA ABILIA WALOKUWA NDANI YAKE NI 370, NA SIO KAKAMA ULIVYOSEMA HAPO KWENYE HILO TANGAZO LAKO USIWAPOTOSHE WATU.

    ReplyDelete
  2. Abiria waliku mia mbili na thelatini na tisa ukijumuisha pia na wafanyakazi wa kwenye ndege hakuna kilichopotoshwa, anonymus 1 umechanganya na namba ya flight ambayo ni 370.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...