Mkuu wa wilaya ya Lindi,Dr Nassor Ally Hamid
akifungua mafunzo kwa wanahabari na waratibu wa NHIF/CHF wa mkoa wa
Lindi,Kushoto ni Meneja Nhif Lindi,Bi Fortunata Kullaya na kutoka
kulia ni Bw Faustine Nzota,Mshauri wa Mfuko wa Afya na anaefuata ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Wilaya ya Nachingwea,Christopher Lilai.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi akitoa taarifa fupi
kuhusiana na mfuko huo katika mafunzo ya wanahabari na waratibu wa
Mifuko ya CHF na NHIF Lindi.
Mratibu wa CHF wilaya ya Liwale akichangia kuboresha
mfuko huo katika mkutano wa mafunzo kwa wanahabari na waratibu.
Washiriki wa Mkutano huo.
Na Abdulaziz Video,LINDI
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na Mfuko wa Afya ya
jamii (CHF) mkoani Lindi,imeanza kutoa mafunzo kwa waandishi wa
Habari na waratibu wa Mifuko hiyo,ili kuboresha utendaji kazi ili
kutatua changamoto za Afya kwa jamii ya wakazi wa mkoa huo.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi katika Mafunzo hayo,Meneja wa (NHIF) mkoani
hapa, Fortunata Raymond Kullaya ameeleza kuwa mafunzo hayo
yaliyojumuisha waandishi wa habari na waratibu kutoka Halmashauri zote
sita za mkoa huo yamelenga katika kuboresha utendaji wa kazi na
kubaini changamoto mbalimbali zinazokwamisha jamii kujiunga na mifuko
hiyo ukiwemo wa Afya ya Jamii(CHF).
Aidha alibainisha kuwa wanahabari wanashiriki vizuri katika
kuhamasisha na kuwapa wananchi taarifa muhimu, zikiwemo za kujiunga na
Mifuko hiyo ya (NHIF na CHF) ili kuwaondolea usumbufu pale
wanapokwenda kupata huduma za matatibabu pale wanapougua.
Kullaya pia alisema kuwa Ofisi yake imeona upo umuhimu wa kuwapatia
mafunzo hayo ili wanahabari waweze kuielimisha jamii iweze kubaini
fursa zitakazowezesha utatuzi wa Changamoto hasi na chanya za huduma
sanjari na kubadilishana uwezo wa kiutendaji baina yao na watumishi wa
mifuko hiyo.
Kullaya akataja sababu nyingine ni pamoja na kuwapa elimu ya
mabadiliko yaliyotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya pamoja na
maboresho yaliyokwishatekelezwa hivi karibuni na kuwa na kauli moja.
"Kama mjuavyo ugonjwa unapokwenda kwa mwanadamu haupigi hodi,hivyo
muda unapokujia huna pesa za kujitibia,Bima yako itakusaidia
kukuwezesha kupata matibabu sehemu yeyote hapa nchini kwetu"Alisema
Kullaya.
Akifungua Mafunzo hayo,Mgeni Rasmi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya
Lindi,Dr Nassor Ally Hamid aliwataka Waratibu wa Mifuko hiyo
kuhakikisha dawa zinapatikana na Wahudumu wa Afya wanakuwa na Lugha
Mzuri kwa wagonjwa wanaowahudumia ambapo pia aliitaka ofisi ya NHIF
Pia kutumia viongozi mbalimbali wa Serikali katika kuhamasisha
kutokana na Idadi ndogo ya Jamii kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii
ambapo kwa mkoa wa lindi ni asilimia 6.6 tu ndio iliyojiunga na mfuko
huo.
Katika kupunguza makali ya Tiba katika hospital za Binafsi licha ya
kuwa na gharama ndogo za Uchangiaji kwa kaya ambapo unalipa mara moja
kupata huduma za Tiba kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Nae Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Lindi,Abdulaziz
Ahmeid ameahidi kushirikiana na ofisi hiyo ili wanahabari watumie
kalamu zao katika kuhakikisha Jamii inapata huduma stahiki ikiwemo
kushauri pale ambapo kuna changamoto zinazochangiwa na watoa huduma
sambamba na kutoa wito kwa Wanahabari kujiunga na mifuko hiyo badala
ya wao kuhamasisha tu.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyoratibiwa na Ofisi ya Mkoa ya NHIF pia
wito umetolewa kwa zahanati,Vituo vya Afya vilivyopo mkoani humo
kutumia fursa ya kukopa Vifaa tiba kwa mikopo na nafuu Kupitia katika
mfuko huo ambapo malipo yake yatakatwa kupitia madai mbalimbali
wanapowahudumia wagonjwa wa Mfuko wa NHIF
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...