Kituo kikuu cha mabasi yaendayo sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ikiwa haina gari baada ya wamiliki wa magari yaendyo maeneo hayo kugoma kutoa huduma.
Kutokana na mgomo huo ndipo madereva wa magari hayo na makondakta wakaamua kugeuza stendi hiyo uwanja wa mpira wa miguu likapigwa mbungi kati ya madereva na makondakta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nilishasema muda, ni makosa kwa serikali kuachia watu binafsi masuala nyeti. Usafiri ni moja ya suala nyeti kwani jamaa wakigoma na magari yao serikali haiwezi kuwalazimisha. Kwani mtu kitu chake anafanya apendavyo. Ukiangalia hata mataifa makubwa, Marekani, Uingereza, makampuni makubwa ya kusafirisha watu kazini kila siku(mabasi na treni) ni ya umma ingawa wanaweza kuwa wanashindana na makampuni makubwa binafsi. Na hawa ndiyo mabepari wakubwa. Matajiri wenye magari wakigoma kazi zote zingine zinazorota. kwa hiyo ubepari unaweza kuwa ujamaa kwa mfano niliousema hapo juu.
    Mmbongo Chiberia.

    ReplyDelete
  2. Naona taratibu tunageuka kuwa jamii ya migomo,Kila mtu anataka afanye anavyotaka.Meno ya serikali yako wako?

    ReplyDelete
  3. Haya mambo yote ni kero kwa wananchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...