Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akibonyeza kitufe cha kuchezesha droo ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti mapema leo katika ofisi za Kiwanda cha Bia chaa Serengeti jijini Dar es Salaam, huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha  Tanzania Bakari Maggid(kushoto) na Afisa Mwandamizi kutoka PWC Golder Kamuzora(kulia). 
Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akizungumza na wana habari wakati wa droo ya saba ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kuchezesha droo hiyo mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam na kulia kwake ni Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bakari Maggid.


PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZIL NA SERENGETI INAENDELEA.
Washindi Zaidi kupatikana, zawadi za ving’amuzi na simu za kisasa zazidi kutolewa!

26 Machi, 2014: katika hafla fupi mapema leo kampuni ya bia ya Serengeti imeendelea kuchezesha droo zake za winda safari ya Brazil na Serengeti na leo washindi wawili wa simu za kisasa aina ya Samsung galaxy tablet wamepatikana. 

Kwa mtu kujishindia zawadi zetu unahitaji kununua chupa ya bia ya Serengeti na kuangalia chini ya kizibo ambapo utakuta bia ya bure au tarakimu 6 ambazo utazituma kwa ujumbe mfupi kwenda namba 15317 ambapo utapata ujumbe ukikujulisha kama umejishindia fedha taslimu kati ya shilingi 5000 na shilingi 10000 na pia namba yako itaingizwa katika droo ambapo utaweza kujishiandia king’amuzi, simu ya mkononi au tiketi ya kwenda Brazil.

Mji wa moshi katika maeneo ya majengo umepata bahati ya kutoa washindi wawili wa simu aina ya Samsung tablet. Juma lililopita katika droo ya 6 ya winda safari ya Brazil washindi wawili waliopatikana wote wanatokea katika maeneo ya Majengo Moshi. Droo hiyo ilishuhudiwa na waandishi wa habari, ofisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, PWC pamoja na Push mobile media. Droo kubwa itatoa tiketi ya kwenda Brazil ambaponmshindi atalipiwa gharama zote kwa siku atakazokaa huko.

Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo aliongea na mshindi wa kwanza Bw Matei Kleti Mofulu kutoka Nyakato, Mwanza. Akiwa na furaha muda wote wa maongezi alisema hajaamini kama ameshinda na amekuwa akiamini michezo hii siyo ya ukweli ila Serengeti wamemfumbua macho kuwa ni za kweli. 

Mshindi wa pili pia alipokea habari hizi kwa furaha na kusema kuwa ni muda kuwa wa kisasa kwa kutumia simu ya kisasa. Pia mshindi wa pili wa simu ya kisasa Bw Godwin Paul ambaye ni mwanajeshi wa JWTZ aliishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa zawadi hiyo na kuwashauri watumiaji wa Serengeti kushiriki katika promosheni hii.

Tafrija fupi za kugawa zawadi kwa washindi zimeendelea katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania ambapo katika juma lililopita mshindi wa simu ya kisasa wa Dar es Salaam alikabidhia zawadi yake katika maenao ya kimara. Mshindi huyo Bw Erick Mazigo alishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwa waaminifu kwa wateja wao na kuwapa zawadi zao. Promosheni ya winda safari ya Brazil ambayo imekuwa gumzo nchi nzima imeshapata washindi Zaidi ya 100000 wa bia za bure, Zaidi ya washindi 13000 waliojipatia fedha taslimu shilingi 5000 na 10000.

Kunywa kistaarabu; washiriki wanatakiwa kuwa na umri wa Zaidi ya miaka 18; vigezo na masharti kuzingatiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...