Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kibindu,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo leo Machi 16,2014.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI,CHALINZE.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana na wanakijiji wa kijiji cha Kwamsanja,wakati alipofika kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwaomba kura katika Uchaguzi huo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kwaruhombo,leo Machi 16,2014.Ridhiwani Kikwete ameahidi kuyashughulikia Matatizo mbali mbali wanayokabiliana nayo Wananchi wote wa Jimbo la Chalinze,yakiwemo ya Barabara,Maji,Elimu,Matibabu na mengine mengi ambapo amesema atayafanyia kazi atakapopewa ridhaa ya kuwa kiongozi wa Wanachalinze.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini Mlemavu wa miguu,Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo,ambaye alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kulembelea kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana.Ridhiwani ameahidi kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea Mlemavu huyo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja dogo katika Kijiji cha Chang'ombe,linalounganisha Barabara inayotoka Kwarihombo kupitia Kwamsanja mpaka Kibindu,Kata ya Kibindu,ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 16,2014.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kada wa Chama cha Mapnduzi Ridhwani, hakikisha ktk ahadi zako kwa wananchi ule msemo wa ''uzee mwisho chalinze'' unakatiwa rufaa na mpaka wa uzee unahamia Morogoro!

    ReplyDelete
  2. Duuh ama kweli! wakati wakuomba kura unaweza ukafanya vitu ambavyo hujawahi fanya! Kazana kijana..

    ReplyDelete
  3. hongera kwa ushindi wa kuwania ubunge chalinze kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Ridwan Kikwete.... ...tuko pamoja kwa mabadiliko kwa wana chalinze

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...