
zilizopo.
Hiyo imefanya serikali kuchagua wale wenye uelewa wa juu pekee
kujiunga na shuleza elimu ya juu, huku wale ambao pengine kwa bahati
mbaya wamekwama kufikia alama zilizowekwa na serikali, wakiokolewa na
shule binafsi.
Hii imesaidia idadi kubwa ya watoto nchini kupata elimu ya sekondari
tofauti na miaka ya nyuma ambapo watoto wengi waliokuwa wakifeli na
kukosa shule basi huishia nyumba.Shule za Filbert Bayi, nazo ni miongoni mwa shule binafsi zilizokuwa na mchango wa pekee, hususani katika elimu ya sekondari.
Miaka tangu kuanzishwa kwa shule ya Sekondari Filbert Bayi, na miaka
sita ya mahafali ya kidato cha nne, imeweza kuonyesha maajabu ya aina
yake kwa kufuta kabisa daraja sifuri.
Shule ilianza ikiwa na wanafunzi 28 na hadi sasa wamefikia 380, na
Mkurugenzi wa shule hizo Anna Bayi anasema wamefikia idadi hiyo kwa
sababu ya kuchagua watoto wanaokidhi viwangovilivyowekwa na shule.
"Tungekuwa tunachukua watoto wa kila aina, basi nadhani idadi ingekuwa
kubwa zaid, lakini kwanza hatupokei watoto we na wenye utovu wa
nidhamu na wenye uelewa wa hali ya chini.
Anasema ingawa wanachangamoto ya kuachiwa watoto wasio na uelewa
sana, kwa kuzingatia wote wanaofanya vizuri kuchukuliwa shule za
serikali, lakini bado wameweza kutoa watoto bora kielimu.
Hata hivyo, nao huwachuja na kupata wenye uelewa wastani, na tangu
wameanza kufanyamitihani yakidatocha nne hawajawahi kupata daraja
sifuri.
"Tulianza kwa kupata dara la nne, ambapo walikuwa wachache sana,na
tulishuka hadi akabaki mmoja, na mwaka jana hatukupata daraja la nne,
na badala yake daraja moja na mbili ndio walikuwa wengi huku daraja la
tatu wakiwa wachachekabisa,"anabainisha.
Kutokana na matokeo hayo, shule ya sekondari Filbert Bayi iliyoko
Kibaha mkoani Pwani, imefanikiwa kushika nafasi ya sita kimkoa, kati
ya shule 105,na nafasi ya 71 kitaifa kati ya shule zaidi ya 3000 na
nafasi ya nne kiwilaya.
Pamoja na mafanikio hayo, lakini shule hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kubwa ya kunyoosha maadili ya watotona hatimaye
kuwa wamoja.
Shule binafsi zina mchango mkubwa sana katika nchi yetu. Mwanafunzi yoyote mwenye afya nzuri akipata mazingira mazuri na vifaa vya kusoma anaweza kufaulu.
ReplyDeleteMwandishi anaandika utafikiri tuko 90s...kwa sasa wanaoenda shule binafsi si waliokosa nafasi sababu ya ufaulu...ila ni wenye fweza kwa kuwa shule binafsi nyingi zina kiwango cha ubora wa juu ukilinganisha na za serikali....
ReplyDeleteMimi hii inaniumasana...enzi za Mwalimu tulikuwa tunasoma sana ili tufaulu kwenda shule za serikali...
Kwa sasa wanangu wanajua kabisa watasoma saint sijuhi nini maana shule za serikali si dili tena....
Huu ni mwanzo wa matabaka...watakao kuwa na bright future ni wenye ela si akili....