Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud Chawene wakikata utepe kwa pamoja kuzindua kisima hicho cha Maji.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya akiongea na wafanyakazi wakituo cha Afya  Tunduma mara baada ya kukabidhiwa kisima hicho na TBL.
Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.

Kituo cha Afya Tunduma

Kampuni ya Bia Tanzania imetoa msada wa kisima cha maji kwa ajili kituo cha Afya Tunduma chenye thamani ya shilingi milioni 24 chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa.

Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.

Malulu amesema kampuni yake imetenga jumla ya shilingi milioni 450 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha yenye nia ya kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Naye Afisa mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa amesema mradi huo utasaidia kumaliza  tatizo la maji hivyo kuwa faraja kwa wagonjwa wanaotumia kituo hicho ikiwa ni pamoja na raia wa nchi jirani ya Zambia.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  amesema kuwa watahakikisha wanautunza mradi huo ili uwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho .

Aidha Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka ameshukuru Kampuni hiyo kwa kutoa mradi huo na hivyo kuwataka wahudumu kuitunza miundo  mbinu  ya maji. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo ameitaka kampuni ya bia kupanua wigo wa kusaidia Nyanja nyingine kama vile elimu ili kufanya mji wa Tunduma kuwa na maendeleo zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...