Mfanyaakazi wa Idara ya Masoko wa Kampuni ya Vodacom Albert Maneno (wa tatu kushoto) akiongea kabla ya kukabidhi Sh. 2 milioni kwa askari wa kikosi cha Usalama Barabarani Moses Alphag (wa kwanza kushoto) aliyeibuka kidedea katika program ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari hao jijini Dar es salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM. Fedha hizo zimetolewa na wafanyakazi wa Vodacom pamoja na wananchi mbalimbali walioguswa na programu hiyo. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova,akipokea sh 2 Milioni kutoka kwa Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Albert Maneno zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom na wananchi mbalimbali kwa ajili ya askari wa kikosi cha usalama barabarani Moses Alphage aliyeibuka kidedea katika program ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari hao jijini Dar es salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akimkabidhi Askari wa usalama barabarani ,Moses Alphage fedha taslimu Sh. Milioni 2 zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wasikilizaji wa kituo cha Redio Clouds FM kupitia program ya kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalam barabarani jijinidar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio. Alphage huongoza magari katika daraja la Mlalakuwa, Kawe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana afande. Vodacom tunaomba mdhamini ufungaji wa taa kwenye vituo vya mabasi ili kupunguza uhalifu. Asanteni Vodacom kwa kujali.

    ReplyDelete
  2. Ni motivation nzuri ya afisa wa usalama barabarani, itahamasisha wengine kufanya kazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...