Mfanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink Maria Chundu akiteta jambo na Bi.Khadija Sultan (78) wa kituo cha kulelea wazee cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala mara walipotembelea kituo hicho kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika kituo hicho.Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
Mhasibu wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Joyna Mwafute akimlisha chakula mmoja wa wazee waishio katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo kilakala Bi.Tabu Juma( 65) wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipofika kituoni hapo kutoa misaada wa vyakula,mafuta ya kula,blanketi na mashuka vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
Meneja Mafunzo na Uendelezaji wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink,Maxine Makenzie, akimpatia soda mmoja wa wazee wasiojiweza wanaotunzwa katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo kilakala jijini Dar es Salaam,wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipofika kituoni hapo kutoa msaada wa Vitu mbalimbali vikiwemo mashuka,blanketi na vyakula mbalimbali kwa wazee 45 waishio katika kituo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani wazee hao msiwape soda(sukari) sio nzuri kwa afya hususani wazee wenye rika hili. Maji ni kinywaji kizuri zaidi kuliko soda.
    Dr. MsemaKweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...