Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula kulia akimkabidhi Funguo ya Gari Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael,kushoto ni Elizabeth Lukaza Mchambuzi wa Shirika la UNDP Tanzania.Hafla imefanyika leo Wizara ya Biashara Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula kulia akimkabidhi Vifaa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael katika hafla iliyofanyika leo Wizara ya Biashara Zanzibar
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian Raphael kulia akitoa neno la Shukran baada ya Makabidhiano ya Gari na Vifaa kwa Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula.
========= ======= ======
Na Makame Mshenga
-Maelezo Zanzibar.
-Maelezo Zanzibar.
Wizara ya Biashara na Viwanda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi Gari na Vifaa vya Ofisini kwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Wizarani Malindi mjini Unguja.
Msaada huo uliofadhiliwa na Shirika la Biashara la Dunia WTO ulitolewa ili kuijengea uwezo Wizara ya Biashara ya Zanzibar katika kukabiliana na majukumu yake ya kila siku.
Akikabidhi Msaada huo Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Bara Edward Sungula kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael amesema Suala la Biashara ya Kimataifa ni la Muungano hivyo Serikali mbili lazima zishirikiane na kusaidiana katika kutekeleza majukumu yao.
Amesema Msaada huo ni utekelezaji wa Mradi wa “Capacity Building for Trade Development and Integration Project” ambao una lengo la kuzijengea uwezo Serikali katika kutekeleza misaada chini ya utaratibu wa “AID FOR TRADE”.
Ameongeza kuwa msaada huo ni mwanzo wa kudumisha ushirikiano katika kutekeleza mradi huo na njia ya kuendeleza kudumisha Muungano uliopo baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian Raphael ameishukuru Wizara hiyo juu ya Msaaada huo na kuongeza kuwa utachochea ufanisi katika majukumu yao.
Katika kutekeleza Mradi huo wa kukuza Sekta ya Biashara Tanzania Bara na Zanzibar Mradi umeanza kwa kununua Vifaa ambavyo ni pamoja na Gari mbili, Komputa, Projekta na Mashine ya Kuprintia.
huyu jamaa wa maelezo zanzibara sijui hajui vugezo vya uandishi wa habari. maana kwa sasa hakuna wizara ya biashara na pia hakuna wizara ya biashara huko bara. uandishi kaaazi kwelikweli
ReplyDelete