Katika siku zilizopita suala la uraia pacha lilikuwa gumzo kwa Watanzania waishio kwenye Diaspora na wale waishio Tanzania. 
Lengo kubwa la gumzo au mjadala huu lilikuwa ni kujadili kama uraia pacha unaweza kuruhusiwa kwa raia yeyote wa Tanzania au kwa mtizamo mwingine, na lengo ni kuelimisha umma kuwa mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania na atakayepata uraia wa pili hawezi kupoteza haki yake ya kuwa Mtanzania. 
Suala hili bado linajadiliwa na Watanzania lakini bado wapo Watanzania wanaopinga uraia pacha kwa kudai kuwa Watanzania waishio ughaibuni hawana uzalendo au “patriotism”. 
Nimeonelea ni vizuri kulijadili suala hili la uzalendo kwa vile Watanzania wengi wa ughaibuni na wale waishio Tanzania bado wanaamini kuwa si kweli kuwa Watanzania wa Ughaibuni hawana uzalendo na hapa natoa mifano iliyotolewa katika kuthibitisha ukweli huu. 
 Kwa kuanzia ingekuwa vizuri dhana ya uzalendo ieleweke vizuri. Pili, dhana ya nani ni mzalendo na nani si mzalendo itawekwa bayana na mwisho, namna ya kupima uzalendo wa Watanzania waishio Tanzania na nje ya Tanzania itaelezwa kwa kifupi. 
 Tunaanza na uzalendo na umaana wake. Uzalendo yaani “patriotism” ni hali ya kuwa mtii kwa taifa kwa maana ya kutii, kulinda na kutetea misingi iliyounda taifa. Kwa kifupi kabisa na bila kuchanganya mambo uzalendo ndio huu. 
Kwa mantiki hii, kuilinda na kuitetea misingi iliyounda taifa na hata kuhakikisha kuwa taifa halifi humfanya raia awe mzalendo. Lakini raia anaweza kuwa mzalendo kwa taifa lake na kutokuwa mzalendo kwa serikali au chama tawala. Na anapokosa uzalendo kwa serikali au chama tawala anaweza kubakia mzalendo kwa taifa lake. 
Mantiki ya kuwa na vyama vingi vya kisiasa ndio hii. Hivyo uzalendo huwa ni kwa taifa na sio kwa chama au serikali tawala. Kwa kuelezea hili, mimi mwandishi wa article hii sina chama cha siasa na naomba nisieleweke vibaya kwa chama tawala cha CCM kwa sababu natoa mifano tu ambayo inapatikana duniani kote na sina vita na CCM wala serikali yake na sina vita na chama chochote cha kisiasa. 
Natoa tu maelezo ya kiutaalamu, kwa sababu mimi ni mtaalamu wa masuala haya. Neno uzalendo yaani “patriotism” lilishika hatamu wakati wa kale ambapo nchi na serikali zililazimisha raia wafuate dini moja kwa misingi ya kujenga taifa na utaifa. 
Watawala walifikia hata kuwauwa wale waliokataa kuwa na dini ya kitaifa hasa kule Ulaya. Na mtu aliyefuata dini ya nchi ambayo kwa kawaida ilikubalika na serikali au watawala alionekana kuwa na uzalendo kwa nchi yake na yule aliyekataa kufuataa dini inayotambulika na nchi na serikali alionekana kukosa uzalendo. Baada ya usumbufu huu, baadhi ya raia wa Mataifa ya Ulaya walipinga mfumo huu na walipigania masuala ya dini na siasa yatenganishwe. 
Na kwa nchi za Ulaya ndipo ukawa mwanzo wa kutenganishwa kwa dini na siasa. Kwa lugha ya kitaalamu kwa mazingira ya Ulaya tunasema “separation of church from the state”, ili kila mtu apate uhuru wa kuabudu. Kwa nchi za Kiafrika, uzalendo uliongezeka sana wakati wa kumfukuza mkoloni kutoka kwenye ardhi ya Afrika. 
Kila Mwafrika alikuwa na lengo na dhumuni moja, kukataa kutawaliwa. Na kauli mbinu ya Waafrika ilikuwa moja na ilisikika katika kona zote za bara la Afrika kauli hiyo ilikuwa ni “Uhuru” ambayo ilisemwa katika lugha tofauti za Kiafrika. 
Kwa mfano, hata Afrika ya Kusini wakati wa “Apartheid” uzalendo uliongezeka na raia waliungana kuupinga kwa nguvu zote wakiwapinga makaburu. Kwa Tanzania, uzalendo uliongezeka wakati wa vita vya kumng’oa Nduli Iddi Amini na wakati wa nguvu kazi wakati wa vijiji vya ujamaa. Uzalendo vile vile hupotea. 
Raia anayeishi ndani au nje ya nchi anaweza kuwa au anaweza vile vile kukosa uzalendo. Mifano ni kama ifuatayo. Kama kuwa mzalendo ni kuwa mtii kwa taifa lako na kuilinda misingi ya taifa lako, pale raia au afisa wa serikali anapokuwa mbadhirifu wa mali ya umma ana uzalendo? Nadhani jibu ni la hasha au hapana. 
 Mtu huyu au afisa huyu hana uzalendo. Kumbe raia aliye “corrupted” hana uzalendo kwa taifa lake. Na raia huyu anaweza kuwa anaishi ndani au nje ya mipaka ya nchi yake lakini kwa kuwa sio mwaminifu kwa taifa lake, anakuwa si mzalendo. 
 Mfano wa pili, raia aishie ughaibuni ambaye ni mtii kwa taifa lake na hayupo “corrupted” na anayesaidia ndugu zake kwenye nchi aliyotokea kwa hali na mali, je huyu sio mzalendo? Jibu ni kuwa huyu ni mzalendo. Nadhani mifano hii ya awali inawafumbua macho kuhusiana na nani ni na nani sio mzalendo kwa taifa lake.Kwa maana hiyo, uzalendo peke yake hauwezi kuwa kigezo cha kuwanyima Watanzania uraia pacha kwa sababu hata Mtanzania aishiye Tanzania na ambaye hajawahi kutoka nje ya nchi anaweza kukosa uzalendo vile vile. 
 Mfano wa mwisho ni kuwa uzalendo vile vile unaweza kupungua au kuongezeka kufuatana na nyakati. Hivyo matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yanaweza kuua au kuhifadhi uzalendo alionao raia. 
Hivyo sio kweli kuwa uzalendo wa kila raia bila ya kujali anaishi ndani au nje ya mipaka ya nchi yake hubakia vile vile maisha yake yote mpaka mauti yamtoe duniani. 
Uzalendo huweza kupungua au kuongezeka au kupotea kabisa. Hivyo suala kumnyima Mtanzania wa ughaibuni haki yake ya kuzaliwa Tanzania na haki ya uraia pacha kikatiba kwa misingi ya uzalendo peke yake ni sababu isiyo na msingi wala umaana wowote. 
 Nadhani kwa maelezo haya dhana hii ya uzalendo inaeleweka na naamini haitatumika kama kigezo cha kimsingi nambari wani cha kuwakatalia Watanzania haki yao ya kiubinadamu ya kupata uraia pachja na haki yao ya kuzaliwa Tanzania inayowapa haki ya kuwa Watanzania kikatiba.  

Imeandaliwa na Deogratius Mhella, 
Katibu wa Vikao vya Viongozi wa Jumuiya za Watanzania na DICOTA kwa lengo la kuelimisha Watanzania kuhusu suala la uraia pacha katika jitihada za Watanzania wa Ughaibuni kuendeleza mdahalo wa Uraia pacha ili Bunge Maalumu la Katiba liweze kuingiza suala la uraia pacha kwenye katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Word. Fair enough!!!

    ReplyDelete
  2. Maneno mengi na marefu hayasaidii kuwarejeshea Uraia wa nchi ya ''Jamhuri ya Muungano wa Tanzania'' mliokwisa opetoza wenyewe bila kulamizimshwa:

    1.MLIPO UPOTEZA URAIA WA TANZANIA MLILAZIMISHWA NA NANI?

    2.KAMA NI UWEKEZAJI NA KUSHIRIKI KTK KUIJENGA TANZANIA, PANA HITAJI MPEWE URAIA WA TZ WAKATI MNAO URAIA WENU WA MAJUU NA ILHALI MKIWA NA NDUGU, UNASABA NA WENGINE WAZAZI WENU WATANZANIA?

    3.KAMA MLIWEZA KUTUMA DIASPORA REMMITTANCES , MASHINDWA NINI KUTUMA MITAJI NA KUSHINDANA KTK UWEKEZAJI WA MITAJI HUKU TANZANIA NA MABAPARI WENGINE WA DUNIA?

    Mjaribu kuishi kwa kujiamini na kujitegemea na sio kuishi kwa kutegea tegea!

    ReplyDelete
  3. WE STRICKLY SAY NO TO DUAL CITIZENSHIP!

    Uraia Pacha Tanzania hapana labda mjaribu Kenya, Uganda na Rwanda !

    ReplyDelete
  4. Bunge la Katiba lipo busy na suala la Muungano ndio kwanza Wapinga Muungano wamechanwa jana kavukavu, wamemwagwa kinyesi, wametolewa stimu na wametolewa 'Ganzi' kabisa kwa kutolewa hadharani kwa Hati HALISI ya Muungano hadi wakatoka nje ya BUNGE KWA AIBU NA GHADHABU!

    Suala lenu la Dual Citizenship bado lipo pending na hakuna hata dalili kama mtafikiriwa tena, zaidi zaidi MTEGEMEE MAJIBU HASI KWA KUWA MTAMWAGWA KAMA WAPINGA MUUNGANO NA WAPENDA SERIKALI 3 WALIVYOCHANWA VIPANDE VIPANDE JANA!.

    ReplyDelete
  5. Aluta Kontinyua eee?...INGIENI MSITUNI BASI...

    Kisa nini Uraia Pacha eee?,

    Aluta Kontinyua siyo?, je mlipoteza vipi Uraia wa Tanzania?

    Ingineni msituni muone cha moto!

    ReplyDelete
  6. Mlikwisha fafanuliwa ya kuwa 'KUZALIWA TANZANIA SIO KIGEZO CHA KUWA MTANZANIA''

    Si mliona watu wengi sana waliobebwa na Operesheni Kimbunga na kurudishwa Burundi, Uganda na Rwanda walizaliwa na wengine kuzeekea Tanzania?

    Lakini siku ilipofika usiku wa manane Malori ya JWTZ yaliwasili vijijini kwao wakabebbehswa magodoro yao, ndoo, birika, mikeka na mabakuli Maafande wakawasweka ndani ya malori hadi mpakani Usiku huohuo wa manane wakawashusha na mafurushi yao vichwani wakawasha Tochi za mawe 12 na kuwaelekezea mbele waendelee na safari kuduri nchini kwao!

    ReplyDelete
  7. Mjitahidi na Maombi yenu ya Uraia Pacha Kipindi hiki cha Mr.Nice Jakaya Kikwete!

    Mkichelewa mtaula wa Chuya, mnaweza kukuta Prof. Mwesiga Baregu (pinzani mkubwa wa Uraia Pacha) MSIMU UJAO WA SERIKALI YA AWAMU IJAYO amehamia CCM na amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani,,,HAPO KIZA KITAKUWA KIMETANDA URAIA PACHA MARIJOOO!

    ReplyDelete
  8. Ahhh wapi?

    Mliona mwaka jana hadi Raia wa Ujerumani, Norway, Japan na Denmark walinaswa kwenye Operesheni Kimbunga wakiwa wakazi haramu kwa kuishi nje ya Sheria nchini itakuja kuwa ninyi Madiaspora?

    Tanzania sasa imesha kuwa Uswisi ya Dunia mmesha chelewa sana mmeachwa na Basi la mwisho kuelekea maisha Bora!

    ReplyDelete
  9. Haya maombi yenu ya Uraia Pacha msinge yafanya muda huu, mngeyafanya nyuma ya mwaka 2008 wakati Tanzania haijaingia katika orodha ya nchi zenye Utajiri duniani.

    ReplyDelete
  10. Tutatoa Uraia kwa Raia wapya kama Wahindi ambao ni potential Madakitari, na Wafanya biashara wenye mitaji ya maana, lakini sio ninyi Wasanii Madiaspora msio aminika ambao wengi wenu mmeondoka nchini na kuomba Visa kwa Kufoji na Kughushi ktk Ofisi za Ubalozi!

    Na zaidi ya hapo mlipofika nje mkapoteza Uraia waTanzania kizembe.

    Au mnataka kumfanyia Usanii tena Jakaya Kikwete?

    Ohoooo, mutafungwaaaaaa!!!

    ReplyDelete
  11. Mdau Mhella, hii pointi nzuri sana na inaeleweka. Asante sana kwa kuelimisha umma. Atakapinga nadhani atakuwa hakuielewa hii article au ana msimamo wa kutopenda uraia pacha. Hongera mkuu. Asante sana kwa article hii.

    ReplyDelete
  12. Baada ya kupata Uraia wa Majuu ama Makaratasi na Sheria na kupoteza Utanzania:

    -mlijipongeza,
    -mkawaona waliobaki Bongo wajinga,
    -mkawa mnawacheka walio baki bongo,
    -mkajiona wajanja,
    -mkajiona kwenye maisha kila kitu mmemaliza!,

    Ya Mwenyezi ni mengi, mwingi wa miujiza na mwenye makubwa, LIKAWA NI GWARIDE AMBAPO KAMANDA ANAPOTOA AMRI 'NYUMAAA GEUKA' BASI WA MBELE ANAKUWA WA NYUMA NA WA NYUMA ANAKUWA WA MBELE!

    na hivi sasa ni kama gwaride 'WA MAJUU ANAKUWA MACHINI NA WA MACHINI ANAKUWA MAJUU' sijategemea kabisa kwenye maisha yangu hawa jamaa wanaojiita wamepanchi kwa kuwa Majuu kuja kutulilia humu kila kukicha bila kuchoka wakiomba kurejeshewa Utanzania walio upoteza ama Uraia Pacha!


    Na sasa mwishoni mnakuja kuzinduka ya kuwa Utanzania nao una thamani kubwa sana.

    ReplyDelete
  13. mlikwisha uharishia Utanzania na Pasipoti yake sasa mnautaka wa nini tena?

    kwa mtu mwenye akili inayofanya kazi vizuri na kuona mbali hawezi kuchukua maamuzi magumu, ya hatari kama ya kuupoteza uraia kirahisi namna hiyo, kwa kigezo cha kusoma na kuishi nje ya nchi kirahisi.

    hapa ndipo tunapo waona jinsi Madiaspora mlivyokuwa watu wa kutapatapa kimaisha, msio jiamini kimaisha daima, watu wa kujistukia na tamaa mbele huku mkiwa hamna akili za kufikiri mbali!

    ReplyDelete
  14. mimi ninapo fikiria suala la kuupoteza Uraia wa Tanzania ama kuukana Utanzania damu zinanisisimka!

    bora nife masikini kuliko kupoteza Utanzania!

    ReplyDelete
  15. Akili fupi mwisho wake ndio huo.

    Kukana Uraia ni tendo la kuogopesha sana, lakini kwa kuwa mna mioyo yenu ni migumu mliukana na kuupoteza Utanzania!

    Ninyi Madisapora ni sawa na watu wanao jilipua kwa mabomu kujitoa muhanga kama Magaidi.

    ReplyDelete
  16. ujanja mwingi mbele kiza!

    kazi kwenu kurudisha Utanzania wenu.

    ReplyDelete
  17. Jamani nawaambieni kila siku wabongo wachache wanopinga uraia pacha, hawaoni mazuri wenyewe kila kitu ni kibaya. Ujinga, wivu, na fitina vinatumaliza wabongo. Wasi wasi wenu na Diaspora ni nini? Wakuu,Mh. Kikwete na Mh. Membe, wamelisema linapita. Nyie misukule ya mitandaoni kataeni mpaka mapovu yawatoke, maisha bado yatakwenda ni nyinyi mtakaokosa kitu. Kweli elimu ya nguvu inaitajika kwa ndugu zetu hawa(kama kweli wapo).*Mmbongo Chiberia*

    ReplyDelete
  18. Unaweza kuta Wanaocoment kuukata sio wengi ila ni mtu mmoja au wawili wanajaza micoment.
    He/she got to be a sworn hater.either alirudishwa hm toka majuu au maisha ya mbele yalimshinda au hajawai hata toka tz na aliomba visa akanyimwa.
    Au ni njemba aliyechukuliwa dem wake kipenzi na mtu wa mambelezz.

    ReplyDelete
  19. Majuu njaa kali, ndio maana ninyi Madiaspora wenyewe mnataka Uraia wetu Tanzania wakati sisi hatuna hata haja na Uraia wenu wa Majuu!

    Nchi za Western zimeyumba kiuchumi na yale mambo ya Ukimbizi na Kazi Majuu sasa hakuna!

    Ho Mabepari wenu, Waajiri na Wadhamini wenu huko Majuu wanahamishia Mitaji kwenye nchi kama Tanzania, itakuwa ninyi muweze kuihsi huko?

    ReplyDelete
  20. Uraia Pacha hamuupati ng'o!

    ReplyDelete
  21. Nyie wapinga uraia pacha, naona akili zenu zimeganda. Hamna kitu cha kufanya?! Kwa mijadala kama hii hamna haja ya kubishana na nyie, naona nyie ndiyo wenye nchi, si ndiyo maana mko busy kuigawa nchi? Hamna kitu hapo, Dar. yenyewe lazima ujue kuongelea.Jamaa wanopigania kurudi ni kuwasadia nyie masikini jeuri, mie wala sina hamu na nyie viumbe. Piganeni, ongeni kwa kejeli hamtabaki masikini kwa ajili ya akili zenu mgando. Narudia tena, hamna kitu hapo, na hicho hicho kisochopo, mtakilipua sasa hivi, ni kichekesho viumbe nyie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...