Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt. OwdenburgMdegela |
Wachungaji na msaidizi wa Askofu kulia wakifuatilia salam za pasaka zilizokuwa zikitolewa na askofu Dkt. Mdegela |
Waumini wa KKKT usharika wa kanisa kuu Iringa leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA |
Na Francis Godwin, Iringa
ASKOFU mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt. OwdenburgMdegela ameitumia ibada ya Jumapili ya Pasaka leo kulaani vikali wale wote wanaowatukana waasisi wa Taifa hili Sheikh Abeid Amani Karume na Mwalimu hayati Julius Kambarage Nyerere.
Askofu Dkt Mdegela amesema kuwa watu hao wanapaswa kuwaomba radhi watanzania huku akisisitiza wajumbe umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kurejea bungeni ama kufungasha virago vyao na kurudi nyumbani kwao na sio kuzunguka kupandikiza chuki kwa wananchi.
Askofu Dr Mdegela aliyasema hayo leo wakati akitoa salam za pasaka kwa waumini wa Dayosisi hiyo kupita washarika wa kanisa kuu.
Dkt. Mdegela asema "Watanzania tunataka kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani na kuanza kutafuta kuvuruga amani na utulivu wetu ambayo ni lulu ya pekee inayogombewa na nchi nyingine na kuwa wanaotaka lulu hiyo ivurugike wasivumiliwe kamwe.
"Kinachofanywa bungeni kwa sasa ni mzaha wa hali ya juu na Watanzania wanapaswa kuwachunguza vema wawakilishi wao hao wakiwemo wabunge wa vyama vyote na wale wanaoeneza mbegu ya chuki wasichaguliwe tena...."
Asema wajumbe wa bunge la katiba hawana sifa ya kutengeneza katiba kwani wametanguliza mzaha na matusi yasiyo na tija na kuwa hawa wanaokwepa bunge na kutaka kuzunguka kwa wananchi wanapaswa kuzuiwa kufanya hivyo na vyombo vya usalama kwani wanataka kuipeleka nchi pabaya.
"Kama wamekula pesa za wananchi kwa muda wote huo kwa ajili ya kuunda katiba iweje leo watoke bungeni na kudai kuja kwa wananchi mikono mitupu??" amehoji.
"Wananchi tuwakatae wajumbe wanaotaka kuzunguka kupandikiza chuki kwa wananchi kwa kujiita wao wapo kwa ajili ya katiba ya wananchi hali wamekimbia bunge na kutaka kutuwakilisha nje ya bunge
"....tunawakataa wao na mawazo yao na pia kama wajumbe wa bunge hilo wameshindwa kazi tutaikataa rasmu ya katiba ambayo italenga kutugawa watanzania.
"Na niweke wazi mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba mbali ya kazi hiyo bado tunawajibu wa kumrekebisha pale alipokosea kwani Wazanzibar wa Pemba wanataka serikali nne sio tatu mbona hajaeleza
" ....nasema serikali mbili ni jibu kama haiwezekani bado tuwe na serikali moja itakayotuunganisha"
Hata hivyo Dr Mdegela alisema kuwa msimamo wake na waumini wa kanisa hilo ni kuwa na serikali mbili na ikiwezekana kuwa na serikali moja pekee na si vinginevyo na iwapo wajumbe wa bunge la katiba wameshindwa kazi na kugeuza bunge hilo ni sehemu ya kuonyeshana ujuzi wa kutukanana ni vema wakirudi katika mwelekeo mzuri ama kurudi majumbani kwao ili viongozi wa dini mashekhe na maaskofu wakaifanya kazi hiyo ya kuunda katiba bila kutukanana .
"Nimejizuia sana kwa kipindi hiki cha bunge la katiba nisiseme chochote ila kutokana na mambo jinsi yanavyokwenda uvumilifu umenishinda nimelazimika kusema na ninachosema nimekiandika ili wale wapotoshaji washindwe kupotosha ninachosema....wayahudi walikataa kuongozwa na Samweli kwa sababu walisema watoto wa Samweli wanatabia mbaya ...walikataa kuongozwa na Mungu kwa madai kuwa na wao wanataka mfalme wetu uli tukienda kupigana na watu ili tuwe kama mataifa mengine ila Mungu hakutaka wao kuwa kama mataifa mengine ila wao wanataka kuwa kama mataifa mengine ....Samweli akaenda mbele ya Mungu akilia ....ila Mungu akasema hawajakukataa wewe wamenikataa mimi ...enyi watanzania tukikataa lulu tuliyopewa na Mungu ya kuwa nchi ya amani tutakuwa hakuwakatai viongozi wetu tutakuwa tunamkataa Mungu"
Aliwataka watanzania kuyatazama mataifa jirani kama Kenya ambao walijipenda wao na kushindwa kuwapenda majirani sasa Wasomari wameingia wanawasumbua ila tazameni pia Malawi ambao walimtaka rais wao awe Joys Banda ila alipoingia tu Ikulu alitangaza ndoa za jinsia moja pamoja na nchi ya Kongo ambayo imesaidiwa na Tanzania kurudi katika amani ikiwemo nchi ya Burundi ambayo Rais wake amekuwa akishinda katika maombi kwenye kanisa lake na kuacha kuongoza nchi.
"Tunapaswa kujiuliza amani hii iweje leo ichezewe na watu wachache wenye uchu wa madaraka na hata kususa bunge la katiba ...hatujifunzi kutoka nchi za majirani zetu kama Uganda ,Rwanda kuna vyama 10 vya upinzani na kuna vikundi 10 vinavyotaka kumpindua Rais huku Uganda kuna mtu anaitwa Kony yeye siku zote kumshumbua Rais ....ninyi ni nani Tanzania bara na visiwani mkaa kwenye amani kiasi hiki na mnakataa umoja na kuanza kuwasikiliza wanaopandikiza mbegu ya kuvuruga amani ya kutaka serikali tatu ....watanzania tunataka kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani"
Dr Mdegela alisema kuwa hadi sasa mwenendo wa bunge la katiba unatia aibu kubwa kwa Taifa na hata nje ya taifa hili na kuwataka wajumbe hao kuwa wasikivu na kama walisema wanakwenda kuandaa katiba ya wananchi iweje kabla ya kuanza kwa bunge hilo walianza kwa kulilia posho kuongezwa hali wakijua walimu hawajalipwa malipo yao pamoja na wafanyakazi hawajaongezwa mishahara yao.
"Natamka wazi kuwa mimi Dr Mgedela sina imani hata kidogo na wajumbe wa bunge la katiba .....kama wanavyoonekana na walivyo wana hadhi ya kutoridhika watatuletea katiba mbovu kwa sasa na wao ni wabovu ..
"Natamka rasmi kuwa tume iliyoandaa rasmi ya katiba haukuandaa msaafu wala Biblia ili andaa kitu ambacho mbacho kinaweza kuhojika na kukataliwa ama kukubalika wao si Miungu ni wanadamu kama sisi madai kuwa wanavyeo vingi serikalini hata mfagiaji anavyo ....sasa naiomba serikali hao waliojitoa bungeni wanataka kuja kwa wananchi tunasema hatuwataki ....
"Hivi kama mtu ameshindwa kujenga hoja bungeni watakuja kutueleza nini nawaombeni usalama wa Taifa fanyini kazi ya kulinda amani yetu ....kama hawataki kurudi bungeni basi waende majumbani kwao"
Askofu Dr Mdegela alisema kanuni za bunge wametunga wao na iweje leo wanakimbia kanuni waliyoitunga hivyo kama wanaona kanuni ni mbaya basi watuombe Watanzania wenye akili tuwasaidie hata yeye anaweza kwani wajumbe hao ni walafi wasiopenda amani ya nchi hii.
Katika hatua nyingine askofu huyo alisema kwa sasa kinachoendelea na kuwa kila kanda itataka serikali yao iwapo hoja ya serikali tatu ikapitishwa.
well said doctor Mgedela! Hawa ukawa wanachezea lulu tulioachiwa na waasisi wetu.. Ankal kama una video ya hii speech naomba uitupie humu jamvini tafadhari.
ReplyDeletemdau,
ughaibuni
sawa baba askofu tumekusikia hayo ni mawazo yako na ni haki yako au kama ya kanisa lako pia ni haki yenu kuyatoa sharia za nchi hazikatazi fikra tofauti,sawa iwe za binafsi au taasisi.
ReplyDeletehuku Zanzibar na sisi tuna shehe wetu wa msikiti mkuu wa kidongo chekundu nae anataka serekali tatu hayo pia ni mawazo yake au ya msikiti wetu na ni haki yetu kwa mujibu wa katiba na sharia ya nchi hii ya Zanzibar hakatazwi mtu au taasisi yoyote kutoa fikra zao.
sasa twendeni tukawaulize wananchi wenyewe wanatka serekali ngapi?
wanasiasa na viongozi wa dini wote tunajua misimamo yao hilo sio geni kilich kigeni ni wananchi wa nchi hii hawajaulizwa wanaogopwa nini?
mdau.
Zanzibar.
The mdudu,acheni kuwasemea wananchi coz wananchi wenyewe wanajua kinachoendelea kwasababu wao ndio wenye MATATIZO MAKUBWA KWENYE HII NCHI,nyie mnaosemea wananchi mkumbuke yakwamba mnafanya kazi na mnalipwa mishahara minono na wala kitu njaa kwenu hamjui ni nini,ndio maana sisi wananchi tunataka serikali 3 zenye kuwajibika na nidhamu pasipo na RUSHWA,serikali mbili za sasa zimeshindwa kuleta usawa kwa wote,ndio maana kuna gepu kubwa sn kati ya MASIKINI NA MATAJILI,matatizo ya sisi masikini haya hapa,Hatuna maji safi majumbani mwetu,Hatuna umeme,Hatuna shule za maana,Hatuna hosipital za maana,Hatuna kazi za maana hizo sababu tosha kabisa sisi makabwela kuzitaka hizo serikali 3,hayo matatizo niliyo ya sema hapo kwenu nyie hayapo hasa nyie viongozi na vyama vyenu ndio maana mnazitetea hizo serikali 2,ila sisi hatutaki tena hizo mbili.
ReplyDeleteAskofu mwenye akili timamu na asiye tumiwa na chama chochote hawezi kutoa kauli ya kuwa huo ni msimamo wa kanisa lake. Hilo ni kosa, sababu katika kundi la hao waumini wake pia kuna wanao penda serikali mbili, tatu au moja. Angesema hayo ni mawazo yake. Msimamo wa kanisa lake ni ile imani yao, sababu ndio iliyowaunganisha. Sasa wakitokea waumini wengine wa kanisa hilo wakasema wanataka serikali tatu atawafukuza katika hilo kanisa? Hayo ndio matatizo ya kuwa wachungaji kisha mnahudhuria mikutano ya ndani inayoongozwa na makada wa chama fulani, sababu mkutano uliitishwa na mkuu wa mkoa. Mnalamba posho na kupewa masharti ya kwenda kutoa tamko kwenye ibada zenu yanayo lingana na matakwa ya vyama hivyo. Shame on you. Mnachanganya mambo ya kaisari na Mungu. Na Shehe mkuu wa mkoa huo akitangaza msikitini kwake yeye na msikiti wake msimamo wao ni serikali tatu. Je hapo hamuja leta mgawanyiko mkubwa katika jamii?
ReplyDeletebwana askofu nafikiri kazi yako ni kutuongoza sisi kiroho , hizi siasa tuziache kwa wanasiasa, na kuhusu serikali ngapi tunazitaka au muungano tunautaka basi waulizwe wananchi wa pande zote mbili kwa kura ya maoni , wewe huna haki baba askofu kutuambia chochote kuhusiana na serikali , na mikifanya hivyo mtawafanya na mashehe kule znz na hapa bara waanze kuzungumza siasa misikitini kuelimisha waumini wao ,
ReplyDeleteAsante sana mdau. Wananchi ndio waamuzi wa mwisho katika kura ya maoni. Mengine yote msemayo ni mawazo yenu binafsi.
DeleteChonde ccm msilete uchakachuaji kwenye hili
Baba Askofu big up! Hao UKAWA ni wanafiki, wachochezi! Wanahubiri Utanganyika? Huo ni ukabila!! Hawana tofauti na Makaburu. Msikilize yule Toto Tundu Lissu, msikize mtoto si rizki Jussa chuki tupu, kejeli, matusi, dhihaka. Muungano wa aina gani wanaohubiri? Tuwakatae makanisani tuwakatae misikitini. Mungu ubariki Muungano wetu.
ReplyDeleteDuh Baba Askofu ulikuwa wapi siku zote? Hawa wana UKAWA Hawana lolote, wameshalaniwa. Leo wanamtukana Nyerere na Karume wana mwisho mwema hao? Hebu wadau angalieni Hansard, mtaona matusi ya Jussa, Abubakari Hamis na wengine . Hawana haja na Muungano . Wao uchochezi na kuhubiri chuki. Hawana nafasi katika Tanzania huru!
ReplyDeleteBravo Baba! Muungano wa serikali mbili ndiyo utakaodumisha amani na umoja. UKAWA wana sema wametoka kwa sababu ya ubaguzi. Hivi kuwaita wenzao Intarahamwe siyo ubaguzi ? Wao wanapandikiza mbegu za chuki: Utanganyika , Uzanzibari, huu si ubaguzi? Kero zipo, zitatuliwe! Serikali Tatu, marais watatu, si ndiyo kero zitazidi? Mzigo huo atabeba nani? UKAWA Hawana sera warudi Bungeni wakatunge Katiba!
ReplyDeleteMimi, naomba kuuliza swali. Endapo wananchi wanatata serikali tatu ni maana yake maraisi watakuwa watatu? au inakuwaje. Na kama maraisi watatu kwa serikali ya Tanzania mbona tutakuwa ni kama sehemu ya kukumbatia madaraka? Sawa, wananchi wanahitaji serikali tatu lakini hatujui madhala yatakayotokea baada ya serikali tatu. Tuongee na kupima mambo, tuamue jambo kwa busara. Mwenye ufafanuzi wa hili naomba anisaidie. Mdau
ReplyDeleteMambo ya Katiba ni masuala ya kisheria. Ni masuala ya raia. Ni makosa watu kutumia nafasi za uongozi wa kidini kuingilia kati mchakato wa raia na mstakabali wa nchi yao.
ReplyDeleteMarekani wana serikali 52 za majimbo na serikali 1 kuu. Mbona hakuna shida. Watu wako selective sana kwenye kujenga hoja. Eti wanatoa mfano wa Urusi ya zamani, Senegal-Gambia etc. Kila nchi ni tofauti.
ReplyDeleteUwepo wa serikali 3 sio matakwa ya wapinzani, bali hayo ni maoni ya wananchi kwa mujibu wa Tume ya Maoni ya Katiba. Hayo ni maoni ya wananchi hata sisi wa ughaibuni tulitoa maoni kwa njia ya mtandao. Iweje kuwasakama wapinzani wakati wao wako sambamba wanaunga mkono mawazo ya wananchi walio wengi, serikali 3 !!. Hawa wanachama wa chama tawala wanaolazimisha serikali 2 kinyume na maoni ya wananchi ndio wanaoleta fujo kwa sababu kuanzia hatua ya mwanzo ya kutoa maoni,maoni ya taasisi mbalimbali, maoni ya mabaraza hadi Tume ilipovunjwa rasmi waaliunga mkono michakato yote na mawazo ya wananchi, Iweje leo waje na mawazo tofauti ya kulazimisha serikali 2!!! wanatuyumbisha sisi wananchi. Basi nashauri mchakato wa maoni ya muundo upi wa serikali unaofaa, uanze upya na kila mwananchi apige kura ya maoni kwanza kujua ni aina ipi ya muundo inayotufaa, na maoni ya wananchi yaheshimiwe, ndipo baadaye tujadili katiba mpya.
ReplyDeleteLinalojitokeza hivi sasa katika duru za uchambuzi wa mchakato wa katiba mpya ni kuwa "HAKUTAKUWA NA KATIBA MPYA".Huu mvutano utaendelea hadi siku ya mwisho wa Bunge hili "utumbo". Maafikiano ya theluthi mbili juu ya tatu katu haitafikia na hata kama ikifikia na katiba to be ipigiwe kura na wananchi haitapa mandate ,matokeo yake basi Raisi wa Jamhuri hataitisha tena bunge la katiba na atatangaza TUENDELEE NA KATIBA TULIYONAYO.Ambapo itakuwa ni ushindi kwa warevu na ni ushindi kwa wajinga.Na wala hapatakuwa na malalamiko kuwa nchi inaongozwa unconstitutional maana katiba ya mwisho itakuwepo na itakuwa ikifanya kazi. Jee ni nani atakuwa mshindi na ni nani mshindwa?
ReplyDeleteSolution ya hili ni kuuvunja muungano tu, watanganyika kivyetu and wazanzibari Kivyao, na kila mtu arudi kwao, enough said.
ReplyDelete