Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Samia Suluhu Hassan akionesha nakala ya Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyothibitishwa Bungeni leo mjini Dodoma.
Juu na chini ni Wajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaounga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoka katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. FITNA KWISHAAA!

    Hawana jipya Ukawa, aibu na ghadhabu zimebakia kwao.

    ReplyDelete
  2. Hapa ndipo tutakapo thibitisha ya kuwa Wapinzani wana Siasa za Kiusanii sana.

    Ukawa mpo kimaslahi binafsi na siyo kwa maslahi yetu wananchi tulio watuma Bungeni.

    Kama Hati ya Muungano mliyodai sana mmeiona na Posho mmesha chukua kwa nini mnasusia Kikao kwa kutoka?

    ReplyDelete
  3. Kutoka kwenu Bungeni watu wa Serikali 3 na Wapinga Muungano NDIYO UTHIBITISHO KAMILI YA KUWA MMESHA SHINDWA RASMI KWA HOJA.

    MUUNGANO UPO TENA KWA SHERIA KAMILI NA SIO MKATABA TU.

    HIVYO TUMEPITISHA SERIKALI 2 NA YOYOTE ATAKAYE LETA UBISHI NI KUPIGWA BUNDUKI AMA KUSWEKWA GEREZANI!

    ReplyDelete
  4. Hawooooo tuwazomeeni Ukawa !

    Hawoooo UKAWA wezi wa Posho za Bunge!

    Yaani wengine Mapadri na Masheikh kabisa kumbe Wezi tu, ama kweli Uumini wa mtu hautegemei kuwa na Suti nzuri ama Kanzu na Kofia ya Kibandiko.

    Kama hamkubaliani na mambo rudisheni Posho mlizo kwisha chukua.

    ReplyDelete
  5. Raisi Jakaya Kikwete alifanya uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba lakini kwa bahati mbaya kwenye msafara wa Mamba Kenge wakawepo, nao ni hawa 'Ukawa'.

    Wachumia tumbo Ukawa haooo wanatoka nje ya mjengo baada ya kukomba Posho zote za mwezi huu hadi 30 Aprili 2014!

    ReplyDelete
  6. Haiwezekani wewe ukawa Padri mzima ama Sheikh mzima halafu ukachukua Malipo ya Ujira wa Posho na kazi yenyewe usifanye!

    ReplyDelete
  7. Tafadhali wajumbe wetu mtumie hekima mnapotoa matamshi mbali mbali. Baadhi ya matamshi tuliyosikia kutoka kwa wajumbe yanaweza kugawanya watanzania. Vyombo vya habari nchini vinaweza kuwa msaada kwa nchi vikiamua kutotangaza matamshi kutoka kwa yoyote yanayoweza kugawanya wananchi au kupanda mbegu za chuki kati yao.

    ReplyDelete
  8. Ukawa mhh siwaelewi hamsomeki kabisaa kususa msuse posho mchukue mko kikazi kweli huko? Kwa ujumla wajumbe walio wengi humo ndanibya mjengo lugha zao ni masikitiko makubwa! Tuliwaamini lakini tunayoyaona na kuyasikia hatuamini macho yetu badilikeni wanenu tutajifunza nini? Nasikia kulia kabisa

    ReplyDelete
  9. Wapinzani wameumbuka, cccm pigeni kazi wanangu achaneni nao tena na wasirudi teeeenaaaa

    ReplyDelete
  10. Ni kweli Ukawa waweza kulaumiwa kwa kususia kikao, Lkn tujiulize Rasimu iliandaliwa ili msimamo wa chama fulani ndio upite au maoni ya wananchi yajadiliwe ili tupate katiba? Tukiwa na jibu juu ya hili, basi na chama chenye watu wengi kisidhanie kuwa katiba ni ya chama. Mimi mawazo yangu ni kuwa wajitahidi kuwa wakweli na wasiweke mbele msimamo wa chama bali wa Taifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...