Balozi wa Tanzania Nchini China,Lt. Jen. Mstaafu Abdulrahaman Amiri Shimbo akimkabidhi Mhe. Rais Xi Jinping hati zake za utambulisho katika hafla iliyofanyika Ikulu “The People’s Great Hall” ya Jamhuri ya Watu wa China, Beijing, tarehe 20 Machi 2014 . Balozi A.A Shimbo alikuwa wa kwanza kuwasilisha hati zake za utambulisho kati ya mabalozi 14 waliowasilisha hati zao siku hiyo.
Mhe. Balozi Shimbo akiwa na Mhe. Rais Xi Jinping mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho Ikulu “The People’s Great Hall”.


Maafisa Ubalozi wa Tanzania Beijing, walioambatana na Mhe. Balozi Shimbo katika tukio hilo muhimu wakisalimiana na Mhe. Rais Xi Jinping. Maafisa hao walikuwa ni pamoja na: Brigedia Jenerali Blasius K. Masanja, Bibi Matilda S. Masuka, Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Bw. Edmund J. Kitokezi, Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mzee Shimbo bila ya shaka ataendelea kupata dozi za kichina za kuzidisha uhai dhidi ya gonjwa linalo msumbua

    ReplyDelete
  2. ANON WA April 24, 2014, na wewe wasumbuliwa na gonjwa gani; la magonjwa ya wengine, ama sivyo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...