Kamera ya Globu ya Jamii,mchana wa leo imeshuhudia vijana hawa ambao hawakuweza kutambulika majina yao mara moja,wakisombelea mchana kutoka katika mtaro wa kupitisha maji kando kando ya barabara ya inayoelekea kwenye hoteli ya White Sands kutokea Afrikana,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam na kupakia kwenye gari kama waonekanavyo pichani.Hali hiyo inapelekea kuchimbika kwa kingo za barabara hiyo hasa pale maji yanapopita kwa wingi pindi inyeshapo mvua kubwa.
 Wengine walikuwa bize kupakia kwenye mkokoteni kama waonekanavyo
 Sehemu ya barabara hiyo ikionekana kumeguka upande kutokana na kuchimbika kwa chini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. The mdudu, kama hakuna usimamizi au sheria za kukataza wacha watu wapige mzigo,mm sijui niseme mara ngapi ili mnielewe nishasema mara kibao ya kwamba hii Tanzania yetu kila mtu hufanya mambo atakavyo kama vile hamna kitu inaitwa SHERIA so twendeni hivi hivi

    ReplyDelete
  2. Mdaumchangia maoni hapo juu yaelekea hukumfaham mtuma picha hizi. Hakuna sheria ya kusafisha mtaro na wala si kosa kuusafisha mtaro,lakini mtuma picha malalamiko yake jinsi gari lilivyoegeshwa na kuwa ni usumbufu kwa magari na vyombo vyengine.Kama wasafisha mitaro wa city wameshindwa kufanya kazi zao jee wasamaria wema wasisafishe na kujipatia riziki zao humo humo?

    ReplyDelete
  3. Kuchota mchanga wa ujenzi barabarani kutaleta mmomonyoko na kuharibu barabara hiyo.

    ReplyDelete
  4. kwa kweli hali hii ya uharibifu wa mazingira ni nchi nzima. kuna barabara zilizosahauliwa kabisa hapa dar tena tunaziita za mjini na uharifu wa aina hii upo hamna anaeweza kuusemea hadi waandishi wa habari wanaporusha kwenye vyombo vya habari ndio wahusika washituke tunaenda wapi sijui nchi hii. Ombi waandishi jaribuni kupita njia ya tabata ukitokea vingunguti wanaita tabata liwiti,hadi maeneo ya barakuda pia barabara za ndani toka segerea (nyuma Ya gereza)inayoenda unganisha kimara kwa kichwa kuna makorogo jamani kama mahandaki au machimbo ya dhahabu but ni barabara hizo na ukusanyaji wa mchanga kwenda kuuza unaendelea kama kawaida utadhani hii nchi haina viongozi wa mitaa. inasikitisha wadau jamani.

    ReplyDelete
  5. Ninyi watoa maoni wa kwanza na wa pili inabidi mfikie maridhiano: mmoja akachimbe mchanga na mwingine akasafishe mtaro.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...