Mhe. Mohamed C. Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa na mwenyeji wake Mhe. Georgina T. Wood, Jaji Mkuu wa Ghana ofini kwake. Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania yuko nhcini Ghana kwa ziara maalum ya kubadilishana ujuzi na Majaji wa Supreme Court ya Ghana.

Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa kwenye ziara ya kubadilishana ujuzi wa utekelezaji wa shughuli za kisheria na Utawala baina ya Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Ghana akiongozana na Mhe. Jaji Kiongozi na Makamishna wa Tume ya Mahakama ya Tanzania. 

Mada kadhaa zitatolewa na zitajadiliwa na kupata uzoefu wa utekelezaji wa majukumu ya kisheria na utawala wa mihimili ya Mahakama kwenye nchi za utawala wa sheria. Miongini mwa mada zitakazo jadiliwa ni pamoja na:-

Taratibu za Supreme Court ya Ghana za uondoshaji wa Mashauri
Uhuru wa Mahakama na mgawanyo wa madaraka 
Majukumu na uwezo wa” Judicial Council” ya Ghana
Mfumo wa upimaji wa utendaji kazi kwa Waheshimiwa Majaji na Mahakimu nchini Ghana
Mfumo wa uratibu wa Mashauri mbalimbali Mahakamani
Utaratibu wa kumaliza Mashauri nje ya Mahakama
Utawala wa Sheria na Haki za Binadamu
Elimu ya sheria kwa umma
Pamoja na mada hizo, ujumbe wa Mhe, Jaji Mkuu utatembea, utaona na kulinganisha utendaji wa taasisi nyingine za kutoa haki kama vile
Mahakama ya Biashara
Mahakama ya Ardhi
Mahakama ya Haki za Binadamu
Tume ya Maboresho ya shughuli za Mahakama nchini Ghana
Financial Court

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...