Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akitoa taarifa ya kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) ofisini kwake leo jijini Dar es salaam. 

Na. Aron Msigwa –MAELEZO,Dar es salaam.

Jumla ya kata 22 katika manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke zitaingizwa katika  mpango wa utengaji wa maeneo maalum (smart area) kwa ajili ya kuboresha usafi wa mazingira jijini Dar es salaam.

Akitoa taarifa ya kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Dar es salaam (RCC) leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema uanzishaji wa maeneo maalum ya usafi wa mazingira unalenga kuondoa shughuli zote zinazofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji kinyume  cha sheria na  kulifanya jiji la Dar es salaam kuendelea kuwa  katika hali isiyoridhisha ya usafi wa mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...