Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mmoja wa baadhi ya abiria waliokwama baada ya barabara ya Chalinze-Dar es Salaam kuharibiwa vibaya na mafuriko
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza wakikagua athari za mafuriko zilizoharibu vibaya barabara ya Chalinze- Dar es Salaam eneo la Ruvu Darajani leo.Mamia ya abiria walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko hayo
i Rais akisalimiana na kuzungumza na wanafunzi na mtoto aliyemfuata na kumsalimia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakikagua athari za mafuriko maeneo ya Ruvu Darajani na Visiga
Picha na Freddy Maro
Katika swala zima la miundombinu,kuna lolote tulilojifunza kufuatia hiki ambacho mother nature imetuletea?
ReplyDeleteTumejifunza kuwa kuliko kununua magari mawili,bora ununue 1 na mtumbwi 1.
ReplyDeleteUkitazama kwenye kurasa za mitandao mingi lawama za kijinga sana zinapelekwa serikalini lakini watanzania wanasahau kuwa hili ni jambo la dharura na sio mipango au matakwa ya serikali na wala hakuna wa kulaumiwa kwa hili.
ReplyDeleteMafuriko yanatokea nchi mbali mbali bila matarajio na yameonekana hata nchi tajiri na zilizoendelea na hakuna hata siku moja serikali ikapewa lawama kwa wakati huu watu hujumuika na kusaidiana kwa hali na mali sisi tupo kwenye kupeleka lawama serikalini kweli ni sahihi? Mifano ipo mingi kwa wenzetu waliokuwa na maendeleo zaidi china na U.S.A wote weshaathirika na mafuriko tulichokiona ni misaada na ushirikiano na sio lawama. Tuache tabia hii ya lawama kwa serikali watanzania wote kwa ujumla na tuelekeze hizi nguvu zetu kwenye misaada yenye tija na kusaidia waliathirika.
CCM mmelitaka jimbo hili kwa udi na uvumba.
ReplyDeleteSasa ni kazi ya kukabiliana na changamoto hizi zinazokuja kutokana na ushindi wa kishindo.
Hivyo miundo mbinu ktk jimbo la Chalinze ni mojawapo ya changamoto nyingi ktk jimbo letu hili.
Mdau
Chalinze
I agree with mdau hapo no 2, probably a family/household needs 4 boats and 10 cars.
ReplyDeleteyaani humu kungekuwa na LIKE ningempa mdau no 2 , umenifurahisha sana ... keep it up
ReplyDeletekuna baadhi ya watu humu AKILI ZAO HAZINA AKILI , yaani mpaka mafuriko mnataka kuingiza SIASA ? sasa mafuriko na CCM vimehusiana vipi hapo ? GROW UP
ReplyDeleteNdugu East African hapo juu hizi siyo lawama za kijinga unavyo sema kwani wote tupo pamoja kujenga nchi hii. Hivi kama serikali ingekuwa makini leo hii Dar ingeshindwa kuwa mji ulio pangika? Leo hii angalia miundombinu ya maji taka, maji safi na mengineyo ni mibovu unataka tusifie? Hata huko U.S.A na kwingine wanafanya kazi ndiyo maana miundombinu yao imetulia.
ReplyDeleteHapa tusidanganyane watanzania, wote tumekosea na inabidi serikali ifanye kazi kwaajili ya wananchi na mali zao. Wananchi wanajenga kiolela, serikali inawaangalia tu, unategemea nini?
Sasa wewe unataka alaumiwe nani? Serikali in a wajibu wakurekebisha miundo mbinu, kukataza ujenzi holela na kuwa na system Nzuri ya kuokoa watu safari wa dharura, but hakuna kitu after 50 yrs of independence
ReplyDeleteIssue hii niionavyo mimi ina sura mbili
ReplyDelete1.Sehemu ambayo Serikali haiwezi kukwepa lawama ni pale iliposhindwa kuwa pro-active,kwa kushindwa kuweka na kusimamia vema sheria za mipango miji na hivyo kuruhusu watu kuvamia na kujenga kiholela.matokeo yake tumekuwa na miji isiyokuwa na drainage systems,accessability ni 0 na matokeo yake nikama hivi,hata jinsi ya kuokoa maisha ya watu wakati wa majanga kama haya inakuwa kitendawili.
2.Ukiongelea the aftermath,hapa ndipo hoja ya mdau East Africa inakuwa relevant.kuwa kunapotokea majanga kama haya ni jambo la busara na ustaarabu kufocus katika kusaidia na sio kubaki kulaumu.
Huu ni mtazamo wangu ...