Kikosi cha timu ya watoto wa mitaani kabla ya mchezo huko Rio de Janeiro, Brazil
 Kipa wa Tanzania akiokoa mkwaju
 Furaha baada ya ushindi.
Kupata chanzo na habari zaidi BOFYA HAPA

Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetinga fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada ya kuichapa Marekani mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Hadi mapumziko Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao 4-0. Bao pekee la Marekani katika mchezo huo ambayo hadi nusu fainali ilikuwa haijafungwa lilifungwa dakika za mwisho.

Kwa matokeo hayo, Tanzania inacheza nusu fainali na Burundi. Mechi hiyo inachezwa leo (Aprili 6 mwaka huu) ambapo Burundi imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika nusu fainali ya pili.

Mchezo huo wa fainali unachezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi  akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.

Katika mechi ya kwanza katika kundi B la michuano hiyo, Tanzania ilicheza na Burundi na kutoka sare ya mabao 2-2.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Haileti tofauti yeyote siku zote Tanzania kuna watoto wengi tu wazuri kwa mpira lakini watacheza wapi hapo Dar jangwani kumekuwa depot ya mabasi, leaders kiwanja cha starehe, Biafra uwanja wa mikutano na sehemu nyingine za wazi wanaoitwa viongozi wame/wanajenga majumba na makanisa timu za mpira zinakwenda kutafuta wachezaji wabovu nchi nyingine ndio maana watoto wengi wanaamua kuimba bongo flava, kina mogela, peter tino, nico/deo njohole, amasha, adolf, Rahim, mkweche na wengine wengi tu walikuwa wanasumbua kote Africa walitoka mitaani na katika mashule hayo hayo....so hao watoto wacheze kombe la dunio au la peponi haileti tofauti

    ReplyDelete
  2. Michuzi kwa habari za haraka ni kuwa wabongo katika fainali wameichapa Burundi kwa magoli 3-1 Na kutawazwa kuwa mabingwa wa dunia.
    Mdau UK.

    ReplyDelete
  3. mbona wachezaji nane tu?watatu wameshaingia mitini nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...