Askofu wa jimbo Katoliki Dodoma,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga (aliyevaa kofia) akibariki kanisa la ujirani mwema la Jumuiya ya Wakatoliki ya MtakatifuThomas More,Bunge mjni Dodoma. 

Ibada hiyo iliyohudhuriwa na Spika Mstaafu,Mhe.Pius Msekwa na Mke wake Mhe Anna Abdallah pia ilihudhuriwa na mke wa Waziri mkuu mama Tunu Pinda pamoja na baadhi ya mawaziri na watumishi wa Ofisi ya Bunge.

Ibada hiyo ilifannyika katika ukumbi mdogo uliopo Gorofani katika ukumbi wa Msekwa uliokuwa ukitumiwa na bunge zamani. Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga ,katika ibada hiyo pamoja na kusali na wana jumuiya ya Wakatoliki wa Mtakatifu Thomas More Bunge,kubariki Kanisa pia alizindua jumuiya hiyo na kusimika viongozi wake pamoja na kutumia fursa hiyo kuagana na wana jumuia hiyo kwa kuwa amehamishiwa Jimbo la Rukwa kuendelea na kazi za kichungaji lililopo Mkoani RUKWA.

 Viongozi walioapishwa na kusimikwa kuongoza Jumuiya ya Wakatoliki ya Mtakatifu Thomas More,Bunge Dodoma ni Mbunge wa Rombo Joseph Selasini (Mwenyekiti) Kwa nafasi ya makamu mwenyekiti alisimikwa mama Kitolina Kippa ambaye ni mtumishi wa Bunge Viongozi wengine ni Didas Wambura (mtumishi wa Bunge) kwa nafasi ya Katibu Mhe.Cecilia Paresso makamu katibu na Carlos Kidiru ambaye pia ni mfanyakazi wa Bunge yeye alisimikwa kama mweka hazina. 

Pia baba Askofu Gervas John Nyaisonga alitumia fursa hiyo kuliombea Bunge na mchakato wa kupatikana Katiba Mpya. Mlezi wa Wakatoliki ya MtakatifuThomas More,Bunge Dodoma ni Spika wa bunge la Jamuhuri ambaye hakuwepo,Mhe.Anna Makinda.
Viongozi wa wakisimikwa kutoka kushoto Mhe.Joseph Selasini M/kiti,Kitolina Kippa Makamu M/kiti,,Carlos Kidiru Mweka hazina na Didas Wambura Katibu.

Wana Jumuiya ya wakatoliki ya mtakatifu ThomasMore Bunge Dodoma wakifuatilia Ibada iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Gervas Nyaisonga.na Deusdedit Moshi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...