Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC,Dr. Stergomena L. Tax amekutana na Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbambwe wakati akiwa katika Ziara ya kikazi nchini Zimbabwe. Pamoja na masuala mengine wamezungumzia umuhimu wa kuendeleza kwa kasi ushirikiano na mtangamano wa kiuchumi katika Jumuiya ya Maendeleo Kusuni mwa Afrika (SADC) ili kupunguza na hatimaye kuondokana na utegemezi. Walisisitiza umuhimu wa kukamilisha Ukanda Huru wa Biashara na kuanzisha Umoja wa Forodha wa SADC, na pia uendelezaji wa miundombinu ikiwa ni vipaumbele, bila kusahau uhimilivu kiusalama na kisiasa.
Rais wa Jamhuri ya Zimbambwe,Mh. Robert Mugabe akimkaribisha Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC,Dr. Stergomena L. Tax,wakati alipowasili Ikulu hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Zimbambwe,Mh. Robert Mugabe akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC,Dr. Stergomena L. Tax,wakati alipowasili Ikulu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...