Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Inyonga, Dk. Adis Koni akimpatia maelezo Kinana na viongozi wengine wa chama na serikali kuhusu kucheleweshwa kwa makusudi kituo hicho kukipa hadhi ya kuwa hospitali ya wilaya,ambapo imeelezwa kuwa ucheleweshwaji huo unafanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,kwani maombi walikwishayatuma Wizarani tangu februari mwaka jana.
Kinana akioneshwa baadhi ya vifaa tiba vya kisasa vilivyotolewa msaada na Mbunge wa Jimbo la Katavi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 Kinana akisalimiana na watumishi wa Kituo cha Afya cha Inyonga, wakati wa ziara yake wilayani Mlele.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Inyonga,wilayani Mlele mkoani Katavi jana jioni.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Maskini huyo mtumishi wa afya kapiga yebo yebo ofisi! Mmmh siku hizi ukiwaona baadhi ya watumishi wa umma mpaka huruma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...