Na Sultani Kipingo
Mabingwa wapya wa Tanzania, Azam FC, wametawazwa rasmi na kukabidhiwa kombe lao na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, katika uwanja wa Azam Complex huko Chamazi, Dar es salaam. 
Hii ni baada ya Azam FC kucheza mechi yao ya mwisho  na JKT Ruvu na kuifunga timu hiyo ya jeshi la kujenga taifa kwa mabao 1-0 
Mshambuliaji kutoka Uganda, Bryan Umonyi, ndiye alifunga bao hilo baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Kipre Tchetche. Watu wengi sana walijazana uwanjani hapo kushuhudia  pambano hilo ambalo halikuwa na kiingilio. Vikundi mbalimbali wakiwemo Wanaume TMK walioongozwa na Mheshimiwa Temba vilitoa burudani.
 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Nahodha wa Azam FC, John Bocco jioni hii baada ya kuifunga bao 1-0 JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mabingwa wakisherehekea na taji lao, sherehe za ubingwa zimeendelea Azma Complex hadi usiku wa manane. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...