Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya akiwa ni mwenye majonzi wakati akisaini kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari.  

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu,eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo taratibu zote zinafanyika hapo.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba Shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu,Mhe. Moshi Mussa Chang'a itafanyika kesho Aprili 22,2014 nyumbani kwake Mbagala na baadae mwili utasafirishwa kwenda kijijini kwao Mkoani Iringa kwa Mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwassa wakati wakiwa kwenye Msiba wa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a,nyumbani kwa Marehemu Mbagala,jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya Waheshimiwa wakuu wa Wilaya mbali mbali hapa nchini wakiwa kwenye msiba wa Mkuu mwenzao wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari,nyumbani kwa Marehemu Mbagala jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni familia ya marehemu Mh. Moshi Chang'a. Mh. Chang'a alikuwa ni mtumishi anayechapa kazi namkumbuka alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kwakweli ni mtu wa watu na alikuwa anafanya kazi kwa uwazi na ukweli. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi na apumzike kwa amani. Mdau Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...