Mbunge Kabati akikabidhi mipira kwa mratibu wa mashindano Rashid Bilo 'Shungu' katika makabidhiano yaliyofanyika katika uwanjwa wa Ipogoro.
Mbunge kabati akifunga mashindano ya Rita Kabati Vijana Cup yaliyofanyika katika Kata ya Ruaha mjini Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati akionyesha uwezo wake kisoka huku mkuu wa wilaya ya Kibonde Venance Mwamoto kulia akishangaa utaalam wa mbunge huyo.
00000000 0000000 0000000
MASHINDANO YA MBUNGE YAMALIZIKA
Na Denis Mlowe,Iringa
MASHINDANO ya kombe la mbunge yanayojulikana kwa jina la ‘Rita Kabati Vijana Cup’ yanayodhaminiwa na mbunge wa Viti maalum kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Rita Kabati, yamefikia ukingoni juzi katika kata ya Ruaha jimbo la Iringa mjini huku mbunge huyo akiahidi makubwa kwa wanamichezo jimboni hapo ikiwa ni pamoja na kuifikisha bungeni timu itakayofanya vema .
Akizungumza juzi wakati wa fainali ya kombe hilo mchezo uliofanyika uwanja wa shule ya Msingi Ipogolo na kuzikutanisha timu za Jamaica Fc na News Boys ,Kabati alisema kuwa ameamua kuanzisha mashindano mbali mbali ya soka kwa vijana kama njia ya kuinua soka katika mji wa Iringa na vitongoji vyake.
Alisema kuwa mbali ya mashindano hayo kumalizika anakusudia kuanzisha mashindano mengine ambayo mbali ya mshindi kupewa zawadi mbali mbali bado timu bingwa ataipeleka bungeni mjini Dodoma ili kutambulishwa na kuhudhuria kikao kimojawapo cha bunge.
Kabati alisema kuwa katika ilani ya CCM inasisitiza jinsi ambavyo itakavyoendeleza sera ya michezo kwa vijana na tayari utekelezaji huo umeanza katika mkoa wa Iringa na maeneo mbali mbali ya nchi.
Aongeza kuwa kama mbunge wa mkoa wa Iringa atahakikisha vijana wanaanzishiwa mashindano ya mara kwa mara ili kuwaepusha na vishawishi mbali mbali kama utumiaji wa madawa ya kulevya pia kuifanya michezo
"Nina mpango wa kuendeleza vijana kimichezo na ikiwezekana ligi kuu kuanzwa kuchezwa mkoa wa Iringa iwapo timu zetu zitafanya vema katika mashindano mbali mbali kama ilivyo mikoa mingine ambayo imeendelea kisoka zaidi" alisema Kabati
Katika fainali hiyo News Boys ilifanikiwa kuchukua ubingwa kwa kuwafunga Jamaica kwa penati 5 – 4 baada ya dk 90 kufungana goli moja kwa moja.
Katika mechi hiyo wafungaji walikuwa Hasan Peng’e kwa upande wa Jamaica Fc na Michael Kalinga kwa upande wa News Boys.
Kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Manispaa ya Iringa, (IMFA) Rashid Shungu alisema kuwa mbunge huyo ameonyesha jitihada kubwa katika kuendeleza soka mjini Iringa na kumuomba kuendelea zaidi kusaidia soka Iringa.
Shungu alisema mashindano hayo yameleta chachu kubwa ya soka katika kata ya Ruaha ambapo vijana wengi wamehamasika na kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika soka na kuwa lazima kuweka mkakati wa kudumu wa kuendeleza vijana hao kisoka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...