Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Amantius C. Msole akifuatilia kwa jambo kwa makini wakati wa mkutano wa Kisekta Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaoendelea katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort mjini Unguja Zanzibar. Mkutano huo unaendelea katika ngazi ya Makatibu Wakuu.
Wajumbe wa Mkutano wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiendelea na majadiliano ya Mkutano huo unaoendelea katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort mjini Unguja Zanzibar. Mkutano huo unaendelea katika ngazi ya Makatibu Wakuu.
Wajumbe wa Mkutano wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaondelea katika ngazi ya Makatibu Wakuu wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kufunguliwa kwa Mkutano huo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort mjini Unguja Zanzibar. Mkutano huo unaendelea katika ngazi ya Makatibu Wakuu.
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa kisekta wa Afya wa Jumuiya ya Afrika umekamilika katika ngazi ya
wataalamu Zanzibar.
Mkutano huu ambao ulianza tarehe 14 Aprili, 2014 na umekuwa ukiendelea kwa
siku mbili na sasa unaingia ngazi ya Makatibu wakuu na utaitimisha na Mawaziri wa Afya tarehe 17 Aprili,
2014.
Pamoja na mambo mengine Mkutano huu umepitia taarifa ya utekelezaji wa maamuzi na maagizo
mbalimbali ya Mikutano iliyopita na pia kujadili masuala ya kukamilisha kwa Mpango Mkakati wa Sera ya
Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,Itifaki ya Afya ya Jumuiya ,kujenga sekta ya rasilimali watu ya Afya
ya magonjwa yanayoambukiza na yasiyoamabukiza, haki, jinsia na afya ya uzazi.
Mkutano huo ulifunguliwa na Bi. Asha Ali Abdallahi, Katibu Mkuu ,Wizara ya Uwezeshaji, Jamii, Vijana
na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye alizitaka Nchi Wanachama wa Jumuiya
kuweka pamoja na kuimarisha sera muhimu kwa ajili ya kuendeleza na kukuza hali ya maisha kwa
wananchi wa Afrika Mashariki.
Naye Mkurugenzi wa Sekta za Kijamii wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki akiongea na
wataalamu wa Mkutano huo alisema kuwa Sekretarieti ya Jumuiya inatumbua Juhudi za wataalamu hao
kwa mchango wao mkubwa katika kuendeleza mtangamano wa Afrika Mashariki.
Aidha Kiongozi wa ngazi ya wataalamu kwa upande wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania Dkt.
Elias M. Kwesi aliwakikishia ujumbe wa mkutano namna Tanzania ilivyo makini katika utekelezaji
na uendelezaji wa Mtangamano na kuwataka wajumbe wa mkutano kwa pamoja kutekeleza sera
na mikakati ya kupambana na magonjwa yayoibuka hususani ikiwemo kitisho cha magonjwa yasiyo
ambukiza.
Mkutano huu kwa sasa unaendelea katika ngazi ya makatibu wakuu na utaitimishwa katika ngazi ya
Mawaziri.
IMETOLEWA NA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...