Wananchi wa mji wa Dodoma wakiangalia sehemu ya madhara ya tukio la moto uliotokea usiku wa kuamkia leo katika baadhi ya maduka yaliopo kwenye Barabara ya Nyerere Karibu na Makao makuu ya CCM mjini Dodoma,moto huo umeteketeza maduka matatu na mgahawa wa New Chick Villa Reustaurant. Maduka yaliyoathirika na moto huo ni Gulio La Mahafa Duka lililokuwa linauza bidhaa mbali mbali kwa jumla na reja reja zikiwamo bidhaa za Bakhresa,Duka la Esheki Investment lililo kuwa likiuza bidhaa za maofisini,vitabu na huduma ya uchapaji pomoja na Duka la madawa la lijulikanalo kama Kavula Pharmacy.Picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii Dodoma.

Wakazi wa Mji wa Dodoma wakiendelea kuangalia maduka hayo huku wengi wao wakiwa hawaamini kilichotokea.
Kila aliekatiza katika eneo hilo akusita kusimama na kuangaria athari hiyo ya moto kwenye Maduka hayo.
Sehemu iliyokuwa na maduka ikiwa imeteketea kabisa kwa moto uliotokea leo Barabara ya Nyerere karibu na Ofisi za makao makuu ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Waokoaji wakihesabu baadhi ya bidhaa walizookoa kutoka stoo ya Mahavaz Gumo.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 21/04/2014.
Hali ya ulinzi na usalama ilikuwa ni shwari na wananchi walisherehekea kwa amani na utulivu isipokuwa kulikuwa na matukio mawili ya moto kuunguza nyumba. 
Tukio la kwanza lilitokea  tarehe 20/04/2014 majira ya 20:30 hrs usiku katika mtaa wa Barabara ya Nyerere “zamani kuu street” mkabala na CCM Makao Makuku Dodoma, nyumba ya biashara yenye maduka mbalimbali iliungua kwa moto na kuteketeza mali mbalimbali na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Pilla, miaka 45, mkazi wa Ipagala, alijeruhiwa kwa moto sehemu za mikononi na usoni na kulazwa Hospitali ya Mkoa Dodoma na kuruhusiwa saa 08:00hrs asubuhi tarehe 21/04/2014 baada ya kupatiwa matibabu.

Maduka matatu yaliteketea kwa moto huo ambayo ni:-
1.          Mahavaz Gumo duka la bidhaa za chakula ambalo linamilikiwa na Frank Pilla, miaka 45, mfanyabiashara mkazi wa Ipagala,
2.          Stationary na M-Pesa liamilikiwa na Esheki Elikana Moshi, miaka 54, mfanyabishara mkazi wa Miyuji,
3.          Malaika Cosmetics, duka la vipodozi linalomilikiwa na Jamila Baduwel, miaka 30, mfanyabishara mkazi wa Area “D” na
4.          Duka moja la Dawa baridi Kavula Pharmacy linalomilikiwa na Mariam Rashidi, miaka 40 mfanyabiashara mkazi wa Chamwino, liliokolewa na zima moto. Uharibifu uliosababishwa na moto huo ni kuungua kwa paa la duka hilo na kuta.

Moto ulianzia katika duka la Mahavaz Gumo na kusambaa kwa kasi katika maduka mengine ya jirani na kuteketeza mali zilizokuwemo. Thamani ya mali iliyoteketea haijafahamika na chanzo cha moto huo hakijafahamika, uchunguzi unaendelea.

Tukio la pili lilitokea majira ya 21:00hrs usiku huko Area “D” Bock R site two Manispaa ya Dodoma, nyumba anayoishi Mh. Amina Makilagi, Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM kutoka Mkoa wa Mwanza ambaye hakuwepo yupo safarini. Vitu mbalimbali viliteketea kwa moto na thamani yake bado haifahamika. Chanzo cha ajali hiyo ya moto bado hakijafahamika, uchunguzi zaidi unaendelea.

Aidha Polisi Mkoa wa Dodoma tunawashikilia wanawake 12 kwa kosa la kujihusisha na biashara ya kuuza miili (Ukahaba).

Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongereni sana Polisi.
    Sasa nchi inabadilika kwa maendeleo. Taarifa hizi zinatupa hamasa ya kushirikiana na Polisi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...