Mradi wa kuunganisha sekta za Wazalishaji matunda, mbogamboga
na wenye hoteli (SECO) unaofadhiliwa na Serikali ya Switzerland
umezinduliwa Jijini Arusha.
Mradi huo ambao lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya watanzania
wanaojihusisha na sekta hizo kwa kuongeza uzalishaji wao na uhakika
wa masoko ya ndani nan je ya nchi, unaanza utekelezaji wake mara ,moja
ukiwa na thamani ya jumla ya Dola za Ki marekani milioni tatu na nusu.
Uzinduzi wa Mradi huo umeshuhudiwa na Katibu Mtendaji wa UNCTAD
Dkt Mukhisa Kituyi, Balozi wa Uswizi nchini Tanzania BwOlivier Chave
na Mkurugenzi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara katika Wizara ya
Viwanda na Biashara Bw Lucas Saronga.
Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dkt Mukhisa Kituyi (Kushoto), Mkurugenzi
wa Idara ya Mtangamano wa Biashara wa Wizara ya Viwanda na
Biashara Bw Lucas Saronga( Katikati) na Balozi wa Uswizi nchini Olivier
Chave(Kulia) wakisaini hati za makubaliano ya utekelezaji mradi wa SECO.
Picha ya pamoja ya wafadhili na wawakilishi wa Serikali ya Tanzania
walioshiriki uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika Jijini Arusha.
Picha ya pamoja ya Washiriki wote wa Mkutano na uzinduzi wa mradi
wa SECO uliofanyika mjini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika
Jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...