ZAIDI ya abiria 40 waliokuwa katika basi la Urio linalofanya safari zake kati ya mikoa ya Arusha na Lushoto, Tanga, wamejeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kupinduka wakati likijaribu kukwepa basi jingine katika makutano ya barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio,inaeleza kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10 jioni jirani kabisa na kituo cha mafuta kilichopo kando ya barabara ya Moshi-Arusha.


Taarifa kutoka eneo la tukio zimesema basi hilo lilipinduka wakati likijaribu kupishana na magari yaliyokuwa yakitokea Arusha ambayo yalianza safari bila ya kuwa na mpangilio hali iliyosababisha kutokea kwa ajali hiyo.
Juhudi ya kumpata Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP Robert Boaz zinaendelea kufanyika ili kuthibitisha idadi kamili ya waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo. Tutaendelea kujilishana kadri taarifa itakavyokuwa ikitufikia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...