Tazama shuhuli pevu hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimueleza jambo Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini,Mh.Ali Mohammed Kessy,walipokuwa wakitembea kwa miguu kufuatia msafara huo kukumbana na changamoto ya barabara mapema jana jioni katikati ya Msitu wa hifadhi ya wilaya ya Nkasi.Ndugu Kinana na Msafara wake ulikuwa umetoka kijiji cha Namanyere kuelekea kijiji cha Mwampemba kusikiliza matatizo ya Wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 100,lakini iliwachukua zaidi ya masaa 12 kwenda na kurudi kutokana na ubovu wa barabara.Ndugu Kinana yuko Mkoani Rukwa,Katavi na Kigoma kwa ziara ya siku 21 ya kuimarisha Chama cha CCM,kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kiwemo na kuzisikiliza kero mbalimbali za wananchi
 Ndugu Kinana akishiriki kuweka mawe sehemu korofi,angalau kusaidia Lori hilo pichani lililolala ndani ya msitu huo kwa siku mbili,wapite nae msafara wake uweze kuendelea na safari.
 Sehemu korofi ya Barabara ikiwekwa sawa ili lori lipite na kisha msafara nao uweze kupita,lakini hata hivyo zilitumika juhudi kubwa kuvusha msafara wa Kinana na hatimae kuendelea na safari ya kuelekea kijiji kingine.
 Kila mmoja akipumua kivyake,baada ya kuvuka salama sehemu korofi ya barabara.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (anaerusha jiwe) akishiriki kuziba sehemu korofi kwa mawe,ili msafara uweze kupita
 Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongoza kuvuka sehemu korofi ya barabara kwa miguu,huku madereva wakipiga hesabu zao namna ya kupita.PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-NKASI RUKWA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Waache washike adamu na wakumbuke kwamba wanachi wa eneo hilo wanapata hayo matatizo kila kukicha. Badala ya kwenda kupiga debe la kura basi watengenezeen hiyo bara bara.

    ReplyDelete
  2. Hatari gari linaweza serereka na kumgonga Katibu Mkuu wa CCM Taifa.

    ReplyDelete
  3. mdau wa pili, umewahi kukaa na kuwafikiria watoto na wananchi wanaoishi sehemu hiyo ni hatari gani zinawafika kila siku? Naona umekuwa wa haraka kumjali katibu mkuu wa ccm lakini hukuainisha lolote kuhusu wananchiwa Tanzania wanaoishi sehemu hizo. CCM na serikali yake ndio waliosababisha kutokuwepo na barabara bora sehemu hiyo na sehemu nyingi tu hapa Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa huyu hii naamini ni mara ya pili sasa msafara wake unajikuta ukisumbuliwa na miundo mbinu mibovu. Tatizo ni kuwa viongozi hawafiki sehemu kama hizi kila mara na hawajali matatizo ya wananchi wa sehemu hizi, kama wanajali basi matatizo haya yangelikuwa yameshatatuliwa zamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...