Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura mjini Chalinze jana.

Na John Bukuku  
Ridhiwani Kikwete aliyekuwa mgombea ubunge uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kupitia CCM ameibuka kidedea kwa asilimia 86.61 katika uchaguzi huo kwa kuwamwaga wagombea wengine kutoka vyama vinne vya upinzani.

Matokeo hayo rasmi yametangazwa usiku wa kuamkia leo April 7, 2014 majira ya saa nane usiku katika shule ya sekondari Chalinze na  Msimamizi wa uchaguzi huo  Bw.Samwel Salianga.

Msimamizi huyo wa uchaguzi  amesema Ridhiwani Kikwete (CCM) amepata kura  20,828 sawa na  86.61%, Mathayo Torongei  (CHADEMA) amepata kura 2,544 sawa na asilimia 10.58, Fabian Skauki  (CUF) 476 sawa na asilimia 1.98, Hussein Ramadhani (NRA) kura 60 asilimia 0.25 na  Ramadhani Mgaya (AFP) amepata kura 186 sawa na asilimia 0.59.
 Bw. Salianga amesema kati ya watu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni watu elfu 92, na waliojitokeza katika zoezi hilo ni watu 24,422 ambapo kura halali zilikuwa 24,047 na  kura 375 zikiharibika.
Wagombea waliokuwepo wakati wa kutangaza  matokeo katika uchaguzi huo na kusaini fomu ya kukubaliana na matokea ni wagombea wa NRA na CCM pekee. 

Aidha Wakizungumza baada ya kupokea matokeo hayo aliyekuwa mgombea wa chama cha NRA pamoja na Ridhiwani Kikwete kupitia CCM, kila Mmoja ameshukuru wananchi na kuahidi kushirikina na wana Chalinze kuleta maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. CCM hongera kwa ushindi Chalinze. Ni wakati wa vijana kuongoza. Hii iamshe vijana wengine kuchukua form nafasi za kugombea zinapojitokeza.

    ReplyDelete
  2. Ameshinda kwa kishindo lakini tunasubiri utekelezaji wa ahadi zake hasa pale alipoahidi kila kijiji kukipatia trekta. Sijui Chalinze kuna vijiji vingapi !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...