KARIBUNI WOTE

Kama mnavyofahamu kuwa siku ya tarehe 26 Aprili, 2014 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza miaka hamsini (50), kwa lugha nyingine ni “Golden Jubilee”.

Katika kuadhimisha sherehe hii kubwa na muhimu, Ubalozi umeamua kuandaa Kongamano la Biashara (Investment Forum) kwa siku ya tarehe 25 Aprili, 2014 pamoja na siku ya terehe 26 Aprili, 2014 kuwa siku ya mdahalo (Scholars' day) mjini Berlin, Ujerumani. 

Madhumuni makubwa ya Kongamano hili ni kuwatangazia na kuwaonyesha umma wa Wajerumani mafanikio mbalimbali yaliopatikana ndani ya muungano wetu kwa kuwaonyesha fursa tulizonazo za biashara katika nyanja za kilimo, utalii, nishati na madani, viwanda, elimu n.k.

Hivyo, Mhe. Philip S. Marmo, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ana wakaribisha Watanzania wote wanaoishi nchini Ujerumani na wale wanaoishi kwenye maeneo ya uwakilishi ya Ubalozi kuja kushiriki kwenye Kongamano la Biashara siku ya tarehe 25 Aprili, 2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni kwenye ukumbi wa Logenhaus, Emser Str.12-13, 10719 Berlin, Ujerumani.

Aidha, Mhe. Balozi ana wakaribisha pia kwenye mdahalo siku ya tarehe 26 Aprili, 2014 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana kwenye ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.

Kwa maeleozo zaidi piga simu:

+49303030800

ASANTENI SANA!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...