Tarehe 3/5/2014 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, hivyo kila sehemu huadhimisha siku hiyo kulingana na mipango yao.
Kwa Mkoa wa Mbeya siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya bonanza kubwa litakalowashirikisha waandishi wa habari pamoja na wadau na baadaye kuwa na tafrija fupi ukumbini majira ya jioni.
Kwa mantiki hiyo basi kwa mwandishi wa habari Mkoa wa Mbeya bila kujali ni mwanachama wa Mbeya Press ama la unaarifiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya kushiriki bonanza hilo litakaloanza majira ya saa mbili asubuhi eneo mtaambiwa.
Aidha kuhusu sherehe ya jioni kwa asiye mwanachama wa Mbeya press Club utapaswa kuchangia gharama za ukumbi lengo likiwa ni kufanikisha sherehe hiyo na kuonesha uhai wetu sisi waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya kwa wadau wetu ambao tutakuwa nao uwanjani.
Mchango kwa Mwandishi asiye Mwanachama wa Mbeya Press Club ni Shilingi Elfu Ishirini tu(20,000/=) kwa kila mtu na mwisho wa kuchangia ni tarehe 30/4/2014 lengo ni kuiwezesha kamati ya maandalizi kuandaa shughuli iliyoenda shule.
Ukiwa na mchango tafadhali wasilisha kwa Joachim Nyambo 0756409597, Emmanuel Madafa 0712199378 au Venance Matinya 0755063513.
Tunategemea ushirikiano wenu katika kufanikisha sherehe za uhuru wa vyombo vya habari duniani May 3, kila mwaka.
IMETOLEWA NA KAMATI YA MAANDALIZI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...