JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA
MKOA
WA RUKWA
Anuani ya simu:”REGCOM” Simu Na:(025)-2802138/2802144
Fax Na. (025) 2802217
Baruapepe: rasrukwa@yahoo.com
|
|
OFISI YA MKUU WA MKOA,
S.L.P. 128,
SUMBAWANGA.
|
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella M. Manyanya (Mb) kwa masikitiko
makubwa anapenda kuwajulisha juu msiba mkubwa ulioukumba Mkoa wetu wa Rukwa wa
kuondokewa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Mussa Chang’a (62)
aliyefariki jana jioni terehe 20 April, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Shinikizo
la Damu na Kisukari.
Mwili wa Marehemu Mhe. Chang’a unategemewa kusafirishwa kesho jioni
kutoka Jijini Dar es Saam hadi nyumbani kwao Mkoani Iringa ambapo mazishi yake
yatafanyika keshokutwa siku ya Jumatano tarehe 23 April, 2014.
Marehemu Mhe. Chang’a alizaliwa Mkoani Iringa Januari Mwaka 1952 na
amewahi kushika nafasi mbalimbali Serikalini na katika Chama cha Mapinduzi
(CCM). Katika nafasi ya Ukuu wa Wilaya amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,
Mbeya, Tabora, Mkalama na Kalambo Mkoani Rukwa ambapo mauti yake yamemfika.
Katika Ngazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewahi kuwa Katibu wa CCM
Wilaya ya Njombe na Iringa Vijijini na Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa.
Marehemu Mhe. Chang’a ameacha watoto watano (5) na Mjukuu Mmoja (1).Watoto
wa kiume 3 na Wakike 2.
Kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Rukwa tunatoa pole kwa ndugu, jamaa,
marafiki, na wote walioguswa na msiba huu mkubwa. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu
awape nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi “AAAMIN”
Imetolewa na:
OFISI YA MKUU WA MKOA
RUKWA
Tarehe 21 April, 2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...