Wahalifu
mtandao wameendelea kubuni aina mpya za kufanikisha uhalifu wa mitandao hasa
katika makampuni. Hili limeonekana kushika kasi katika maeneo mbali mbali na
limeingia katika mijadala na kuwa ni moja ya maswala yaliyo onekana yana haja kufikiswhwa kwa jamii ili kuendelea kukuza uelewa wa makosa
mtandao.
Kwanza
kabisa, Faili lolote ambalo linasomeka na kiambatanishi .exe mfano: umoja.exe
nifaili ambalo limedhamiriwa kuingizwa kuwa ni moja ya program za komputa hivyo
kabla ya kubonyeza aina hii ya mafaili lazima uwe na ujuzi wa unacho kibonyeza
ndicho mahitaji yako au la.
Aidha,
kwa upande wa aina hii ya uhalifu umekua ukitumia vifaa kama USB, au CD na DVD
ambazo muhusika anayetakiwa kudhuriwa anaweza kuvikuta aina hizi za vifaa
kwenye ofisi yake na maranyingi vinakua vimekaa katika sura ya kushawishi
muhusika avichukue.
Maara
baada ya kufanya hivyo kinachofata ni muhusika kuwa na kutaka kujua nini kiko
ndani, na ndipo muhusika atataka kufungua na hapo kunakua na faili/mafaili
yenye majina mfano, Mishahara.exe (ambapo muhusika atajua ni faili litakalo
onyesha mishahara ya wafanya kazi) na huwenda pia ika wa majina mengine mbali
mbali.
Muhusika
anapo bonyeza ili kutaka kuona hiyo mishahara, mhalifu anakua tayari kashaingia
katika komputa yake na kuweza kuanza kuleta madhara punde tu anapo anaza
kutumia mtandao. “mara unapo kua mtandaoni tayari unaongeza wigo la mhalifu
kuweza kukudhuru na unapotoka mtandaoni mhalifu anakua hana tena nafasi ya
kukudhuru.” – Yusuph Kileo.
Hili
ni jambo muhimu sana kulifahamu yakua unapokua mtandaoni tayari unakua si
salama sana na utokapo mtandaoni unakua salama kimtamtandao kutokana na madhara
ya usalama mtandao yanaweza kuonekana na kujitokeza pale tu unapo kua
umejiingiza mtandaoni.
Hivyo,
unapo kuta kitu chochote kama CD, USB, DVD na vingine vyenye mfano wa hivyo
ambavyo hujui vimefikaje au hukuwa umeagiza viletwe kwako eidha mlangoni mwa
ofisi kwenye lift ya ofisi au hata mezani ofisini kwako yako unachopaswa
kufanya ni kuviwasilisha maramoja kwa kitengo cha usalama mtandao “Computer
security department” kwa hatua zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...