Na Mwandishi Maalum

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kwamba itaendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa na Jumuiya za Kikanda katika jitihada za urejeshwaji na uimarishaji wa mazingira ya amani na usalama katika nchi zenye migogoro. 
 Kauli hiyo imetolewa na Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Balozi za Japan, Tanzania na Slovakia. 
 Mada kuu ya semina hiyo iliyofanyika siku ya jumanne katika Ubalozi wa Japani hapa Umoja wa Mataifa, na kuhudhuriwa na wawakilshi kutoka Balozi mbalimbali, watendaji kutoka Umoja wa Mataifa, Mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine , ilihusu Ujumuishwaji katika Ujenzi wa Nchi, Inclusivity in Building States: mkazo ukiwa katika ujumuishwaji katika mchakato wa maboresho ya taasisi za usalama. Inclusivity in secjurity sector reform ( SSR) 
Katika ufunguzi huo Balozi Mwinyi aliwaeleza washiriki wa semini hiyo kwamba, wakati Tanzania ikiihakikishia Jumuiya hiyo ya Kimataifa na hususani Umoja wa Mataifa, wa kuendelea kushirikina nayo katika ujenzi huo wa amani, bado inaamini na ingependa kusisitiza kwamba serikali husika ndiyo inayopaswa kuwa mmiliki na muhusika mkuu wa mchakato mzima wa uboreshwaji wa taasisi za usalama . 
“ Pamoja na mambo mengine, ningependa kusisisitza umuhimu wa dhana kuu ya msingi inayosimamia mchakato mzima wa maboresho ya taasisi za usalama, na dhana hii ni umiliki wa nchi husika katika utekelezaji wa mchakato huu” akasisitiza Balozi Mwinyi.
Aliongeza kuwa pamoja na kwamba serikali husika ndiyo mwenye dhamana na mmiliki wa mchakato mzima wa SSR, itakuwa ni jambo jema kama wadau wengine nje ya serikali husika wakashirikishwa au wakajumuishwa katika majadiliano ya utafutaji wa amani pamoja na mchango wa uboreshwaji wa sekta za usalama kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba wadau wote wanakuwa katika muelekeo mmoja ili kuepusha migongano. 
 Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Tanzania kushirikiana na Japani katika uaandaji na uendeshaji wa semina za aina hii kabla ya kuungana na Slovakia. Pamona na Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kushirikia katika ufunguzi wa semina hii, Manaibu wawakilishi wa Japani, Balozi Kazuyoshi Umemoto na Balozi Igor Vencel Slovakia nao walizungumza. Aidha Bw. Dmitry Titov,katibu Mkuu Msaidizi anayehusika na Masuala ya Utawala wa Sheria katika Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa Bw. Dmitry Titov, ambaye ni k
 Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa  ufunguzi wa semina ya siku moja kuhusu ujumuishwaji katika mchakato wa  uboreshaji wa  taasisi za usalama (SSR), semina hiyo ya siku moja  ilifanyika siku ya jumanne katika  Uwakilishi wa Kudumu wa  Japan katika Umoja wa Mataifa na iliandaliwa kwa ubia kati ya Japan, Tanzania na Slovakia
 Naibu  Muwakilishi wa Kudukumu wa Japan katika Umoja wa Mataifa,  Balozi, Kazuyoshi Umemoto akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya siku moja
 Washiriki wa  kutoka Balozi mbalimbali,  Umoja wa Mataifa na  Asasi zisizo za kiserikali wakifuatialia hotuba za ufungi wa semina  hiyo waliokaa  mstari wa mbele ni watoa mada akiwamo  Bw. Dmitry Titov wa kwanza kulia ambaye ni  Katibu Mkuu Msaidizi anayehusikana  masuala ya utawa wa sheria katika Idara ya Operesheni za Ulinzi wa  Amani  katika Umoja wa Mataifa ( DPKO).
 Balozi Igor Vencel, Naibu Muwakilishi wa Kudumu  wa Slovakia naye akisema machache wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...