Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz na Mwambata Jeshi Brig. Gen. Bishoge wakiwa wamesimama kwa heshima wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa na kwaya ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa. Aliyesimama kwenye podium ni Bw. Samwel Shelukindo, Afisa Mambo ya Nje Mkuu ambaye alikuwa MC katika sherehe hizo.
Mhe. Balozi Naimi Aziz akitoa hotuba katika sherehe hizo.
Mhe. Balozi Naimi Aziz akikata keki ya Miaka 50 na wageni waalikwa. Kutoka kushoto ni Balozi wa Equatorial Guinea, Balozi wa Uganda, Balozi wa DRC, Balozi wa Gambia, Balozi wa Brazil, Balozi wa Mauritania na Balozi wa Misri.
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hiyo.
Siku ya sherehe ya Muungano, Ubalozi uliamua pia kutoa somo la historia ya muungano kwa watoto wa Tanzania waishio nchini Ethiopia. Pichani Bw. Nsavike Ndatta, Afisa Mambo Nje Mkuu wa Ubalozi akitoa somo hilo maalum kwa watoto hao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...