Timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza mashindano ya Mei Mosi 2014 kwa ushindi mnono kwa kuichapa timu ya Alliance One ya Morogoro magoli 46 kwa 7. 
 Mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Jamhuri Siku ya Pasaka uliwachukua Utumishi takribani dakika 10 za mchezo kuwasoma wapinzani wao na kuanza kufunga ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Alliance One walishakubali magoli 23 dhidi ya 5. 
Wachezaji waliofanikisha ushindi huo ni Fatuma Machenga (GS) kwa kushirikiana Mwadawa Twalibu (GA), ambao walifanikiwa kufunga magoli 34 na 12 katika goli la wapinzani wa Utumishi. 
Mara baada ya mchezo huo nahodha wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Elizabeth Fusi alisema kuwa amefurahishwa na matokeo hayo na kuahidi kuendelea kuzitimulia vumbi timu pinzani katika michezo itakayofuata. “Tumepania kuwa mabingwa mwaka huu hivyo tutacheza kwa bidii ili kuhakikisha tunatimiza ndoto yetu” Fusi alisema. 
Naye, Mwenyekiti wa timu ya Alliance One Bw. Charles J. Kung’aro alikiri kuwa timu yake ilizidiwa mbinu za kimchezo na Utumishi hivyo kuwaweka wachezaji wake katika wakati mgumu kimchezo hasa wanaposhambuliwa. “Tuliruhusu wautawale mchezo hivyo ikawa rahisi kwao kutufunga hivyo tumejipanga kurekebisha makosa yetu ili tufanye vizuri katika mechi zijazo” Bw. Kung’aro alisema. 
Mashindano ya Mei Mosi 2014 kitaifa yanafanyika mjini Morogoro kwa kuhusisha michezo ya mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba, riadha, mbio za baiskeli, karata, bao na drafti.
 Mchezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Fatuma Machenga (GS) akigombea mpira hewani na mchezaji wa timu wa Alliance One (GK) katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika  Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Wachezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) na Alliance One wakiwa kwenye harakati za kugombea mpira katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini mjini Morogoro.
 Mchezaji  wa  timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Fatuma Machenga (GS)  akifunga goli  dhidi ya timu ya  Alliance One katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Mchezaji wa timu ya Alliance One (GK) akitoa upinzani kwa Fatuma Machenga (GS) wa Ofisi ya Rais (Utumishi) katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Mwadawa Twalibu (GA) akitoa pasi kwa Fatuma Machenga (GS) katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...